Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI), AbdulRazak Badru ametoa wito kwa watumishi wa Umma kuchangamkia fursa ya uwekezaji kupitia dirisha E-Wekeza linalotarajiwa kuzinduliwa na serikali kupitia mfumo wa watumishi portal hivi karibuni.

Badru Pia ameiomba Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhimiza na kuwakumbusha watumishi wa umma kushiriki katika kuwekeza kwa mwendelezo ili kujiwekea akiba kidogo kidogo Kwa manufaa yao ya Sasa na baadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...