Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na mamilioni ya wafanyakazi kote nchini na duniani kwa ujumla kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, MEI Mosi ambayo kitaifa yamefanyika kwenye Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida, yakiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maadhimisho hayo yaliyohusisha wafanyakazi na viongozi wengine waandamizi akiwemo Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete yaliratibiwa na Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyama tofauti vya wafanyakazi. Benki ya NBC ilikuwa kuwa moja ya wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo  kusherehekea siku hiyo muhimu akiwa sambamba na Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya na Meneja wa NBC tawi la Singida Bw David Mushi

Bw Semunyu  alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye maadhimisho hayo unatokana na kutambua  umuhimu wa siku hiyo kwa wafanyakazi ambao ni nguzo muhimu katika ustawi na ukuaji wa uchumi wa nchini huku benki hiyo ikichangia ukuaji huo kupitia huduma mbalimbali za kibenki inazozitoa kwa wafanyakazi hao na serikali kwa ujumla.

“Katika maadhimisho haya NBC tunaungana na mamilioni ya wafanyakazi wenzetu kote nchini kusheherekea siku hii muhimu sana kwetu sote, kwanza tukiwa kama wafanyakazi, pili tukiwa wadhamini muhimu katika kufanikisha uratibu wa maadhimisho haya na tatu tukiwa kama watoa huduma za kifedha kwa wafanyakazi kupitia matawi yetu yaliyopo kote nchini ikiwemo hapa Singida pamoja na kupitia kwa maelfu ya mawakala wetu kote nchini,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Semunyu, ushirikiano wa benki hiyo na wafanyakazi unaimarishwa zaidi kupitia huduma za benki hiyo zinazotolewa kwa kundi hilo kwa kuzingatia mahitaji yao mahususi ikiwemo kuwatunzia amana zao kupitia akaunti mbalimbali kulingana na machaguo yao pamoja na kuwarahishia miamala.

“Pia tunawapatia mikopo ya muda mrefu na muda mfupi bila dhamana na mikopo hiyo imekuwa na tija sana kwao kwa kuwa inawawezesha kujenga au kununua nyumba, kununua vyombo vya usafiri wa kwenda na kurudi kazini na vitendea kazi mbalimbali. Yote hayo wanaweza kuyafanya kwa urahisi zaidi kupitia huduma zetu zilizorahishwa kidigitali yaani ‘NBC Kiganjani’. Ni kupitia urahisishwaji huu wa huduma ndio maana tunasema ‘NBC Kiganjani, Ukigusa Tu Imooo!’,’’ alisema.

Zaidi  Bw Semunyu alitumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wengine wa benki ya NBC kwa namna wanavyotimiza majukumu yao kwa weledi, ubunifu na ufanisi wa hali ya juu hatua ambayo imekuwa ikiwavutia zaidi wateja wa benki hiyo wakiwemo wafanyakazi wa mashirika na taasisi mbalimbali wanaoitazama benki hiyo kama kimbilio muhimu katika huduma za kifedha.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Meneja wa NBC Tawi la Singida Bw David Mushi alisema katika kuwafikia zaidi wananchi wakiwemo wafanyakazi mkoani humo, benki hiyo pamoja na kuwekeza zaidi kwenye huduma za kidigitali imeendelea kushirikiana zaidi na mawakala wa huduma za kibenki mkoani Singida  ambapo kwa sasa benki hiyo ina jumla ya mawakala 300 mkoani humo.

Akiwasilisha shukrani zake kwa wadau mbalimbali wa maadhimisho hayo mbele ya Rais Samia, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya pamoja na mambo mengine alizipongeza na kuzishukuru taasisi fedha ikiwemo benki ya NBC na wadau wengine kwa jitihada zao katika kufanikisha maadhimisho hayo huku akionesha kuguswa na mchango unaotolewa na taasisi hizo katika kuwahudumia wafanyakazi hao.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo  kusherehekea siku hiyo muhimu akiwa sambamba na Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya na Meneja wa NBC tawi la Singida Bw David Mushi






Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC Wakishiriki maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika mkoani Singida.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (katikati) aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo  kusherehekea siku hiyo muhimu akiwa sambamba na Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya (kulia) na Meneja wa NBC tawi la Singida Bw David Mushi (kushoto)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...