Na. Saidina Msangi, WF, Arusha.
Watumishi wa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali wamehimizwa kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kujituma kwa kuwa ni daraja muhimu kati ya usimamizi wa fedha za umma na mafanikio ya maendeleo ya wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akifungua Mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite Garden, jijini Arusha.
Alisema mkaguzi wa ndani si tu mtathmini wa taarifa za kifedha, bali ni mshauri wa usimamizi bora, anayechangia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha taasisi zinafanya kazi kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia misingi ya sheria, taratibu na kanuni.
‘‘Mafanikio tunayoyaona katika usimamizi wa rasilimali za umma na thamani ya pesa katika miradi ya maendeleo yanaonesha kazi kubwa na juhudi zinazofanywa na wakaguzi wa ndani kutoka katika taasisi za Serikali. Juhudi hizi zinapaswa kuendelezwa kwa kasi zaidi ili nchi yetu iendelee kupiga hatua zaidi za maendeleo chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan’’, alisema Bi.Omolo.
Aidha, Bi. Omolo aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha, kutambua mapema maeneo yenye viashiria hatarishi, na kutoa mapendekezo yanayotekelezeka kwa wakati.
Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuthamini mchango wao na itaendelea kuweka mazingira bora ya kazi kwa kuhakikisha wanapata mafunzo, vifaa na msaada unaohitajika ili kutimiza majukumu yao kwa weledi.
‘‘Katika mazingira ya sasa ambapo Serikali inaendelea kusisitiza mageuzi ya kiutendaji, mapambano dhidi ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, nafasi yenu ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote, wakaguzi wa ndani mna jukumu la kuwa walinzi wa maadili, waangalizi wa utendaji, na washauri wa maboresho ya mifumo ya ndani’’, alisisitiza Bi. Omolo.
Pia Bi. Omolo aliwasisitiza kuweka mikakakati ya kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wakaguzi ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili utekelezaji wa majukumu ikiwemo mafanikio na changamoto ili kuangalia namna ya kuboresha utendaji kazi.
‘’Katika kutekeleza shughuli zetu kuna mafanikio ambayo tumeyapata ikiwemo usimamizi wa taasisi za umma kuona utendaji kazi wao na kutoa uelewa kwa taasisi mbalimbali kuhusu usimamizi wa vihatarishi, kufanya uthibiti katika taasisi mbalimbali, kufanya kaguzi za kiufundi na ufanisi na kaguzi maalumu ‘’, alisema Bw. Magai.
Bw. Magai aliongeza kuwa Idara hiyo itaendela kuwajengea uwezo watumishi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Mkutano huo umewakutanisha watumishi wa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kwa lengo la kujadili mafanikio, changamoto, na njia bora za kuboresha utendaji kazi kwa manufaa ya umma kwa kuhakikisha uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za umma.
Naibu Katibu Mkuu-Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza na Watumishi wa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, ambapo amewasisitiza kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kujituma, katika mkutano wa watumishi wa idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu-Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akiteta jambo na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Sehemu ya Ukaguzi wa Ndani Serikali za Mitaa, Bw. Mwanyika Semroki, katika mkutano wa watumishi wa idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai, akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, kuzungumza na watumishi wa Idara yake, katika mkutano wa watumishi wa idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Sehemu ya Ukaguzi wa Ndani Serikali za Mitaa, Bw. Mwanyika Semroki, akizungumza na watumishi, katika mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite Garden, jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akiteta jambo na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai, katika mkutano wa watumishi wa idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Baadhi ya watumishi wa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa, katika mkutano wa watumishi wa idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Sehemu ya Ukaguzi wa Ndani Serikali za Mitaa, Bw. Mwanyika Semroki, (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa wa Serikali, Bw. Benjamin Magai na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Sehemu ya Ukaguzi wa Ndani Serikali za Mitaa, Bw. Mwanyika Semroki, (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Sehemu ya Ukaguzi wa Ndani Serikali za Mitaa, Bw. Mwanyika Semroki, akizungumza na watumishi wa Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, katika mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Sehemu ya Ukaguzi wa Kiufundi, Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Kenneth Nindie, akitoa mada kuhusu majukumu ya Sehemu ya Ukaguzi wa Kiufundi, wakati wa mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Sehemu ya Ukaguzi wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretariet za Mikoa, Bw. Paison Mwamnyasi, akitoa mada kuhusu ukaguzi wa Wizara Wakala za Serikali na Sekretariet za Mikoa, wakati wa mkutano wa Watumishi wa Idara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Olasite, jijini Arusha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...