Diwani wa Kata ya Mjini Manispaa ya Songea Mathew Casian Ngalimanayo, amesema kuwa jitihada mbalimbali zinazotekelezwa katika sekta ya elimu zinalenga moja kwa moja kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika kata hiyo.

Akieleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020_2025, amesema kuwa kwa kushirikiana na RUWASA na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamefanikiwa kujenga matundu 20 ya vyoo katika Shule ya Msingi Mashujaa ili kuboresha usafi wa mazingira na afya ya wanafunzi.

Katika Shule ya Msingi Majimaji, kata ilishirikiana na Ubalozi wa Ujerumani pamoja na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Damas Ndumbaro, kukarabati madarasa mawili na chumba kimoja cha walimu.

Aidha, katika Shule ya Msingi Mfaranyaki, madarasa matano yaliyoharibiwa na upepo Januari 2021 yalifanyiwa ukarabati, sambamba na uboreshaji wa madarasa matatu na ujenzi wa matundu tisa ya vyoo.

Kwa upande wa sekondari, kata imefanikiwa kujenga madarasa sita ya kisasa na matundu manane ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mashujaa. Pia, Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea imejengewa madarasa sita, mabweni mawili, na matundu 25 ya vyoo.

Diwani Ngalimanayo amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma katika mazingira bora yatakayochangia ufaulu wa hali ya juu. Ameongeza kuwa maboresho ya miundombinu ni sehemu ya mkakati wa kuinua elimu katika kata hiyo.

Ametoa pongezi kwa serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia sera nzuri na usimamizi makini wa viongozi wa juu wa chama na serikali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...