*Mweyenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni ampa kongole Diwani kwa kutekeleza Ilani.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Diwani wa Kata ya Kibada Amin Sambo amesema kuwa Kibada imepata maendeleo makubwa chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Ilani ya CCM katika Kata ya Kibada.
Diwani Sambo aliyasema wakati wa Mkutano wa viongozi wa Matawi na Wanachama wenye lengo la kuonyesha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata ya Kibada.
Sambo amesema miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa Vyumba vya madarasa 15 na Matundu vyoo 40 kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kufanya wanafunzi wote wanakuwa na madarasa ya kutosha pamoja na vyoo.
Aidha amesema katika jitihada hizo zimefanyika kwa kushirikiana na viongozi vitongoji kwa ufatliaji wa kamati mbalimbali katika miradi yote iliyofanyika katika Kata ya Kibada.
Hata hivyo katika utekelezaji huo ni pamoja na kujenga soko la kisasa ambalo limekamilika na changamoto zake zimetolewa fedha zingine sh. milioni 380 kutatua changamoto hizo zilijitokeza baada ya kukamilika.
Hata hivyo amesema kuwa mradi mwingine ni ujenzi wa Barabara Kilomita 11.3 za DMP pamoja na kilomita 1.3 za barabara kwa fedha za ndani na kufanya Kibada kuwa na muunganiko wa barabara zitazochochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi.
Sambo amesema kuwa katika kipindi hiki wananchi na wanacha kuhakikisha wanafanya uhakiki wa daftari la mpiga kura katika kujihakikishia wanapiga kura kwa miaka mitano mingine.
Nae Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kigamboni Yahya Sikunjema amesema kuwa Diwani ameweza kutekeleza ilani ya CCM 2020/2025 kwa asilimia 100.
Sikunjema amesema kazi Diwani ni kuwaletea wananchi maendeleo ambapo Diwani wa Kibada ametimiza wajibu huo.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kibada Mboni Mbegu amesema kuwa kazi yao ni kutaka viongozi wanafanya kazi ambapo diwani wa Kibada amefanya kazi yake kwa weledi katika kutekeleza ilani.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nazar Kirama amesema kuwa uongozi mzuri ni ule kushiriakiana na kuonyesha kinachofanyika ambapo diwani Sambo amefanya hivyo.

Diwani wa Kata ya Kigamboni Amin Sambo akieleza utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni na Viongozi waandamizi wa Wilaya katika mkutano wa Viongozi wa Matawi na Wanachama juu ya utekelezaji wa Ilani kata ya Kibada.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Yahya Sikunjema akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa Ilani ya CCM kata ya Kibada na kupongeza Diwani wa Kibada Amin Sambo.
Diwani wa Kata ya Kibada Amin Sambo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana namna alivyotekeleza Ilani ya CCM 2020/2025 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...