Kampuni ya Hisense Tanzania imetambulisha bidhaa yake mpya sokoni ambazo ni Televisheni ya kisasa ya nchi 116 na Frigi la kisasa ambalo Kwa mara ya Kwanza linaletwa katika soko la Tanzania.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari wakati uzinduzi Wa bidhaa hizo meneja Masoko Wa Hisense nchini Zishan Dewji amesema bidhaa hizo ni moja ya bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na ni mara ya kwanza kuletwa nchini kupitia brand ya Hisense.
"Tukizungumzia tv hii ni moja ya tv za kisasa sana ambazo zinatumia akili mnemba (Artificial intelligence) na kumuongezea Mtazamaji mawanda mapana ya utumiaji" Amesema Dewji.
Ametaja Kwa sasa brandiya Hisense ndio brand Bora Tanzania ambayo kila nyumba inapatikana na pembe ya Tanzania kutokana ubora wake .
Mwelekeo wa Tanzania kuwa moja ya nchi zinazoongoza barani Afrika katika ubunifu
wa kiteknolojia na kuvutia wawekezaji ulidhihirika wazi wiki hii, baada ya kampuni ya
kimataifa ya vifaa vya elektroniki – Hisense – kuzindua runinga kubwa zaidi kuwahi
kuletwa Afrika, yenye ukubwa wa inchi 116, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo si tu uliashiria dhamira ya Hisense kwa soko la Afrika, bali pia ulionesha
namna ambavyo Tanzania inazidi kujidhihirisha kama kitovu cha maendeleo ya
teknolojia barani, kutokana na sera bora za kibiashara, uwekezaji wa miundombinu, na
mazingira wezeshi ya ubunifu wa kiteknolojia.
“Tanzania ilikuwa chaguo sahihi kwa uzinduzi huu,” alisema Bw. Jason Ou, Rais
wa Hisense kwa Kanda ya Mashariki ya Kati, Afrika na India.
“Tunaona namna ambavyo serikali na sekta binafsi wanavyoshirikiana kuimarisha
mazingira ya biashara na ubunifu. Hisense inaamini katika ndoto ya Tanzania ya
kiteknolojia – na ndiyo maana tumeamua kuleta mustakabali wetu hapa.”
Bi. Tahera Karim, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Mars Communications Ltd,
wasambazaji wakuu wa Hisense nchini, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu wa
kimkakati:
“Uzinduzi huu unaonyesha imani yetu kwa Tanzania kama nchi inayopiga hatua
kubwa za kimaendeleo.
Kama Mars Communication, tumejizatiti kuhakikisha
Watanzania wanapata bidhaa bora, za kisasa, zinazowiana na maisha yao ya kila
siku, kwa bei nafuu.”
Kwa upande wake, Bi. Vivi Liu, Makamu wa Rais wa Hisense kwa Mashariki ya Kati na
Afrika, na Meneja Mkuu wa Hisense Afrika Kusini, aliongeza:
“Afrika siyo tu soko – ni chanzo cha mawazo mapya, nguvu kazi, na ubunifu.
Tanzania ni sehemu muhimu ya maono yetu ya muda mrefu, na kazi tunayofanya
hapa ni ya kuendeleza vipaji, kutoa ajira, na kujenga mustakabali bora kupitia
teknolojia.”
Katika tukio hilo, Hisense na Mars Communication walitia saini makubaliano rasmi
yanayothibitisha ushirikiano wao wa kuendelea kufanikisha upatikanaji wa teknolojia
bora na nafuu kwa Watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...