Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati alipotembelea mafunzo ya siku moja ya watendaji hao ambayo yanahusisha waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kutoka Kata zote za Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani. Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati alipotembelea mafunzo ya siku moja ya watendaji hao ambayo yanahusisha waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kutoka Kata zote za Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani. Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Hidaya Gwandu akizungumza
Mapema kabla ya kuanza kikao hicho Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Mei 14, 2025 amemtembelea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge ofisini kwake. Mwenyekiti wa Tume na ujumbe wake wapo mkoa wa Pwani kwaajili ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo linaingia awamu ya pili katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar ukiwepo mkoa wa Pwani pamoja na uwekaji wazi wa Daftari la awali la wapiga kura.
********Na Mwandishi wetu, Pwani
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wananchi kutoka mikoa 16 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar wanaokwenda kuanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu yapili kujitokeza kuboresha taarifa zao pamoja na kutazama daftari la awali la Wapiga Kura lililobandikwa katika vituo walivyotumia kujiandikisha au kuboresha taarifa zao hap[o awali.
Hayo yamesemwa leo Mei 14, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku moja ya watendaji wa Uboreshaji kutroka Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani.
“Niwasisitize watanzania wote katika mikoa hii 16, wajitokeze kuja kuboresha taarifa zao au kuja kujiandikisha kwasababu baada ya hapa Tume haita boresha tena Daftari…litaboreshwa kuanzia tarehe 16 hadi 22 Mei kwa muda wa siku saba,”alisema Jaji Mwambegele.
Aidha, mzunguko wa pili utahusisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025.
Katika hatua nyingine Jaji Mwambegele amewakumbusha watendaji hao wa uboreshaji ambao ni Waandikishaji Wasaidizi na waendesha vifaa vya Biometriki kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya zoezi hilo litakalofanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
“Nawakumbusha tena kama nilivyowakumbusha katika zoezi lililopita, kwamba katika utekelezaji wa zoezi hili mzingatie sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi, muwe wanyenyekevu kwa wateja mtakao kuwa mnawahudumia,”alisema Jaji Mwambegele.
“Zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 kinachoipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi mkuu unaofuata.
Nae Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa amewataka wananchi wa Kibaha na viunga vyake kujitokeza kutazama daftari la awali lililowekwa wazi na kama kuna changamoto waweze kuziboresha wakati huu.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili ulianza kufanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.
Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza ulihusisha mikoa 15, mzunguko wa pili mikoa 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.
Mikoa iliyohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 1 hadi 7 mwaka huu.
Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia Juni 28 hadi Julai 04, 2025.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo 7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.
Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
Mambo mengine ni kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Aidha, kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 11(1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume pia ina jukumu la kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura na kuliweka wazi kwa umma.
Lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni kutoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25 Machi, 2025.
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri wanaoshughulika na Uboreshaji huo wakiwa katika mafunzo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...