Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mwenyekiti Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Jacobs Mwambegele amesema kuwa Tume imekubali kuanzisha Majimbo mapya 8 katika Mkoa wa Dar es Salaam,Dodoma,Mbeya,Simiyu,Geita na Shinyanga pamoja na kubadilishwa kwa majina ya Majimbo 12.
Jaji Mwambegele amesema hayo leo Mei 12,2025,Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Taarifa yake kuhusu Kugawa na Kubadilisha majina ya Majimbo ya Uchaguzi, kwa Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025.
Ambapo amesema kuwa Tume imezingatia zaidi vigezo vinne ambavyo imevipa uzito kwenye mchakato wa ugawaji wa Majimbo hayo ikiwa ni pamoja idadi ya watu, ambapo kwa Majimbo ya mjini kigezo kilikuwa kuanzia watu 600,000 na kwa Majimbo ya Vijijini ilikuwa kuaniza watu 400,000,Uwezo wa Ukumbi wa Bunge wa kuchukua Wabunge wapya,Idadi ya Wabunge Wanawake wa Viti Maalum na Jimbo moja la Uchaguzi kutokuwa katika Wilaya au Halmashauri mbili.
Akibainisha Majimbo mapya yaliyoanzishwa kuwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Jimbo la Uchaguzi la Ukonga limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Kivule,Jimbo la Mbagala limegawanywa na kuanzishwa Jimbo la Chamazi. Mkoa wa Dodoma limeanzishwa Jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Mtumba.
Mkoa wa Mbeya limeanzishwa Jimbo jipya moja,ambapo Jimbo la Uchaguzi la Mbeya Mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uyole,Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limegawanya na kuanzishwa Jimbo jipya la Bariadi Mjini,Mkoa wa Geita yameanzishwa Majimbo mawili ambapo Jimbo la Uchaguzi la Busanda limegawanya kuanzishwa Jimbo la Katoro, Jimbo la Uchaguzi Chato limegawanywa na kuanzishwa Jimbo la Chato Kusini,Mkoa Shinyanga limeanzishwa Jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi Solwa limegawanywa kuanzishwa Jimbo la Itwangi.
Akizungumzia kuhusu Majimbo 12 yaliyobadilishwa majina amesema kuwa moja ya Majimbo hayo ni pamoja na Jimbo la Nkenge ambalo litakuwa Misenyi,Mpanda Vijijini ambalo litakuwa Tanganyika,Jimbo la Buyungu ambalo litakuwa Kakonko,Manyoni Mashariki ambalo litakuwa Manyoni,Singida Kaskazini ambalo litakuwa Ilongero,Manyoni Magharibi litakuwa Itigi,Singida Mashariki litakuwa Ikungi Mashariki,Singida Magharibi litakuwa Ikungi Magharibi,Tabora Kaskazini litakuwa Uyui,Handeni Vijijini litakuwa Handeni,Chato litakuwa Chato Kaskazini na Bariadi litakuwa Bariadi Vijijini.
Ambapo amesema kutokana na kuongezeka kwa Majimbo hayo mapya 8 ya Uchaguzi, hivyo Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 jumla ya Majimbo ya Uchaguzi 272 yatatumika kwaajiki ya Uchaguzi wa Wabunge katika Jamhuri ya Muungano na kati ya hayo 222 yapo Tanzania na Majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar na kuwa orodha yote itachapishwa katika Gazeti za Serikali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...