Na JANETH RAPHAEL -MichuziTv - Dodoma

KIWANDA cha mbolea cha Itracom kimetoa tani 2.8 za mbolea kwa Shirika la Community Development Initiatives Support (CDIS),kwa ajili ya maandalizi ya vitalu vya mafunzo ya horticulture kwa vijana katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.

Hafla ya makabidhiano ya mbolea hiyo,imefanyika jijini Dodoma,huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Kaspar Mmuya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mmuya ameipongeza Shirika la Mapinduzi ya Kijani - AGRA, Kiwanda cha Itracom Fertilizer kwa kusaidia kuinua kilimo hapa nchini haswa kwa vijana kupitia shirika la Community Development Initiatives Support (CDIS).

"Tanzania itazidi kufanikiwa kutokana na Utatu huu wa Serikali, Sekta Binafsi na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali. Huu utatu leo ndio tunaoushuhudia hapa kwenye kiwanda cha mbolea",amesema Mmuya.

Shirika la AGRA kupitia mradi wake wa Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture (YEFFA) imewezesha mradi wa miaka mitatu unaotekelezwa na CDIS kwa zaidi ya Bil 1.06 fedha za kitanzania kwa ajili ya kuwapa vijana wa kike na wa kiume ujuzi, ajira, na fursa za kibiashara kwenye mnyororo wa thamani wa vilimo vya bustani (horticulture).

Intracom Fertilizer Limited, kiwanda kinachozalisha mbolea mkoa wa Dodoma, kama mdau muhimu wa sekta binafsi, imejitokeza kwa vitendo kwa kutoa msaada wa mbolea tani 2.8 ili kuwezesha kuanzishwa kwa vitalu 22 vya mafunzo—16 kwa ajili ya nyanya na 6 kwa vitunguu.

Amesema hii ni ishara ya dhati ya sekta binafsi kushiriki moja kwa moja katika kujenga msingi wa kilimo cha kisasa kwa vijana.

Mmuya ameahidi ushirikiano wa kutosha kwani kwa Dodoma, imetoa kipaumbele kwa sekta ya kilimo,huku akisisitiza Serikali ipo tayari kushikana na vijana kwa ajili ya kukuza kilimo Dodoma.

"Kwa sasa Serikali ya mkoa wa Dodoma ina mpango wa kuanza kilimo cha Apple kama zile zinazopatikana South Afrika, tumepima ardhi na hali ya hewa inaruhusu" amesema Katibu Tawala.

Naye Mkurugenzi wa CDIS,Joseph Laizer ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusimama na sekta ya kilimo, ameishukuru AGRA kwa kuiamini CDIS na kiwanda cha Intracom Fertilizer kwa kutoa mbolea kwa ajili ya mashamba darasa, amesema fursa hii itaenda kuzalisha ajira zenye hadhi na kutengeneza matajiri kwenye kilimo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...