Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa limesema limeimarisha uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) katika shughuli za kukabiliana na majanga kwa kutoa misaada ya uokoaji na kibinadamu,”
Hayo yameelezwa leo Mei 22,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo kuhusu mafanikio ya wizara hiyo.
Waziri Tax amesema Kwa kipindi cha miaka minne, wameshiriki kikamilifu kwenye matukio makubwa ya maafa kwa kutoa misaada ya uokoaji na kibinadamu,” alisema Dk. Tax.
Ameyataja miongoni mwa matukio hayo ni uokoaji katika mafuriko ya Mtwara,kuzima moto katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro,usafirisha misaada na kuokoa wahanga wa mafuriko nchini Malawi,uokoaji katika maporomoko ya matope Hanang’ – Manyara,kuokoa waliopata ajali ya jengo Kariakoo – Dar es Salaam na ujenzi wa nyumba kwa waathirika wa Hanang’ na wakazi waliopisha uhifadhi Ngorongoro waliohamishiwa Tanga.
Aidha, kupitia JWTZ, Serikali imekabidhiwa jukumu la kujenga nyumba 5,000 kwa wananchi waliokubali kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro ambapo hadi sasa, nyumba 2,500 zimekamilika katika eneo la Msomera – Handeni, huku nyingine 1,000 zikijengwa Sauni – Kilindi na 1,500 zikitarajiwa kujengwa Kitwai B – Simanjiro, Manyara.
Kwa upande wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT)katika kuendeleza uchumi na kupunguza mzigo wa gharama kwa serikali, Dk. Tax amesema limechangia jumla ya Shilingi bilioni 2.67 kwa ajili ya malezi ya vijana wa JKT na kutoa gawio la zaidi ya Shilingi bilioni 4.27 kwa Serikali kupitia Hazina.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...