Madaba_Ruvuma.

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeendelea kuisaidia jamii isiyo na uwezo wa kugharamia huduma za mawakili kwa kuhakikisha wanapata haki zao kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro, au kupitia uwakilishi wa mawakili watakaotoa huduma hiyo bila malipo.

Akizungumza mara baada ya mikutano miwili ya hadhara iliyofanyika katika Kata ya Mtyangimbole na kuhusisha vijiji vitatu vya kata hiyo Mtyangimbole, Luhimba na Likalangilo , Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Hassan Linyama ambaye ni mratibu wa Kampeni hiyo kwa Halmashauri ya Madaba.

Ameeleza kuwa kampeni inalenga kutoa elimu juu ya masuala ya kisheria, kiuchaguzi, pamoja na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, amebainisha kuwa kampeni hiyo ni endelevu, na imepokelewa kwa furaha kubwa na wananchi, waliokuwa wakisubiri elimu hiyo kwa muda mrefu,

Amesema matarajio ya kampeni hii ni kujenga jamii inayoishi kwa kufuata misingi ya sheria, haki, usawa na amani, kwani bila haki hakuna usawa, na bila amani hakuna maendeleo hivyo jamii inapaswa kuzingatia misingi ya utawala bora ili kufanikisha maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Madaba Evodia J. Kapitingana, alitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia kwa jamii, ikiwemo vifo, ulemavu na kuporomoka kwa hali ya kiuchumi. Alihimiza jamii kukemea vitendo hivyo na kuwachukulia hatua wahusika kwa kuripoti katika ofisi za vijiji, madawati ya jinsia, au taasisi zinazotoa msaada wa kisheria.

Wananchi wa Kata ya Mtyangimbole Wiligis Luambano, Tatu Faraj na Geofrey Mbilinyi walimshukuru Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama, kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha elimu hii inawafikia, Walisema kupitia kampeni hiyo wamejifunza kuhusu haki zao na namna ya kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia.

Pia walitoa rai kwa Wizara kuendeleza utoaji wa elimu ya msaada wa kisheria, hasa katika maeneo ya vijijini, ili kila mwananchi atambue haki zake na kuzuia vitendo vya uonevu, hasa katika ndoa.

Kampeni hiyo inaendeshwa kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 7 hadi 17 Mei 2025 kwa kata zote 8 katika Halmashauri ya Madaba, chini ya uratibu wa Hassan Linyama, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...