Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Dkt. Moses Kusiluka, akizungumza na maafisa wa Taasisi za Umma na Binafsi kwenye kikao cha mwezi kilichofanika jijini Dodoma Mei 2, 2025.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka ametoa wito
kwa taasisis za Umma na Binafsi
kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuwaamini wakaguzi wa ndani ili
kusadia kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kwa lengo la kusaidia kupunguza makosa yanayosababisha hati chafu na badala yake kuleta maendeleo chanya katika taasisi na Taifa kwa Ujumla.
Balazi Dkt.KUSILUKA ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye
kikao cha mwezi cha maaafisa ukaguzi wa ndani ambapo amesema ni muhimu kufanya
kazi kwa kuzingatia welezdi na kufanya kazi kwa uwazi ili kufanikisha malengo
ya taasisi na Taifa.
Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya wakaguzi wa Ndani
Tanzania (IIA) DKT. ZELIA NJEZA ameziomba
taasisi za Umma na Binafsi Nchini
kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa ndani ili wasaidie kuwapa Elimu juu
uendeshaji wa taasisi hizo ili zifanye
kazi kwenye mlengo sahihi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...