KILOSA: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uchaguzi hauwezi kusogezwa mbele kwani wamejipanga kushiriki uchaguzi na hawawezi kuwa sehemu ya kuvunja katiba, hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wajipange 2030.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ameeleza hayo leo Mei 15 wakati akizungumza na wananchibwa Jimbo la Kilosa na Mikumi katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro akimalizia ziara yake ya siku saba iliyokatishwa kupisha maembolezo ya Mzee Cleopa Msuya.
Makalla amesema hakuna jambo la dharura wala vita la kufanya uchaguzi uhairishwe na wala nchi haipo kwenye vita wala jambo lolote la kutisha kusema uchaguzi ushindwe kufanyika.
Amesema CCM ni chama kinachoheshimu demokrasia na hawapo tayari kuvunja katiba na kwakuwa wenye Chadema hawashiriki uchaguzi wasubiri 2030.
“Wenzetu hawa nimesikia walianza juzi Bukoba, Geita wameenda Mwanza nikasikia Myika na Heche wanasema tunaomba uchaguzi usogezwe mbele mpaka tufanye mabadiliko,” amesema Makalla.
Ameongeza: “hakuna mwenye mamlaka ya kusogeza uchaguzi uchaguzi upo kwa takwa la kikatiba na mimi nawaambia Mnyika na Heche tuko tayari kwa uchaguzi sijui wako wapi, ACT wameanza kuchukua fomu na sisi tumejipanga kwenye chama chetu tunaenda kwenye uchaguzi”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...