Na.Ashura Mohamed -Arusha

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdory Mpango amezitaka Taasisi nyingine za fedha nchini kuendelea kusaidia jitihada za serikali za kuwekeza katika sekta ya elimu nchini,ikiwemo kuendeleza Vijana wabunifu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Akizungumza Jijini Arusha wakati Ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika Ukumbi wa kimataiafa wa kituo Cha Mikutano Cha Kimataiafa (AICC) Jijini Arusha,dkt. Mpango alisema kuwa Udhamini wa masomo kwa vijana wa kitanzania ambao wengi wanashindwa kuendelea na masomo kwa kumudu gharamaa masomo ni muhimu kwa kuwa fursa hiyo ni faida kubwa kwa taifa happy baadae.

Aidha Makamu wa Raisi alisema kuwa serikali inaendelea kuwekeza katika mifumo na miundombinu wezeshi ikiwemo nishati na tehama kwa ustawi wa sekta ya fedha nchini.

Nae Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa yapo mazungumzo ambayo yanaendelea na Kati ya wizara hiyo na Taasisi Tanzu ya CRDB Benki Foundation ya kuendelea kuwawezesha Vijana na yanaendelea vizuri ili kuhakikisha Vijana wa kitanzania wenye vipaji wanaendelezwa nje ya nchini haswa wanaosoma masomo ya Sayansi.

"Hatua tuliyofikia katika kuboresha elimu nchini tutachukua Vijana waliofanya mtihani wa kidato Cha Sita na kufanya vizuri mwaka huu 2025,na kufanya vizuri zaidi katika masomo ya Sayansi na kuwapeleka nje ya nchi kwenye vyuo vikuu mahiri kwenda kusoma degree ya kwanza ya katika masuala ya ajili Unde yaani (Artificial Intelligence) na Sayansi zinazoendana na Masuala hayo."Alisisitiza Prof.Mkenda

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bank Foundation Bw.Martin Warioba alisema kuwa ni dhamira ya benki hiyo katika kuinuia jamii,sio kwa ahadi bali vitendo na mradi huo ni zaidi ya ujenzi wa shule,ni ujenzi wa kizazi kipya.

Hata hivyo Warioba alisema kuwa shule hiyo itakuwa mwanga na matumaini utakaoendelea kuangaza maisha ya watoto wa kitanzania,mwanga wa Elimu Bora,Mazingira salama,na nafasi ya kufikia ndoto zao.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB bw.AbdulMajid Nsekela alisema benki hiyo imekuwa kubwa nchini kwa Mizania ikiwa na Mali za zaidi ya shilingi trilioni 16.6,kwa mwaka 2024 huku ikiongoza na amana za wateja shilingi trilioni 10.9,na utoaji mikopo wa shilingi trilioni 10.4 ikithibitisha Imani ya wateja na mchango mkubwa wa kufadhili katika kufadhili maendeleo ya sekta binafsi na ya umma ndani ya Afrika Mashariki.

Bw.Nsekela alisema kuwa mafanikio hayo makubwa yamekuja kufuatia maono makubwa ya watendaji ambao walitangulia kabla yake,huku Ustahimilivu wa Benki hiyo na Ubunifu wa Hali ya juu katika utoaji huduma vikichangia benki hiyo kuendelea kufanya vizuri sokoni.

Katika hatua mbali mbali za kuwawezesha Vijana Jumla ya Vijana 700 wameshapatiwa Mafunzo ya Elimu ya Fedha na biashara na Mitaji huku serikali ikitenga jumla ya shilingi bil.23,kwa ajili ya uwezeshaji wa biashara changa.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdory Mpango
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB bw.AbdulMajid Nsekela akizungumza Jijini Arusha

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza na wanahisa wa Benki wa CRDB ambao hawapo Pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...