Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
MBUNGE wa Nkasi,Aida Kenan (CHADEMA) amesema anatamani kufa ili wana Nkasi waweze kupata maji kutokana na mradi wa Ziwa Tanganyika kusimamia ambao ungepeleka maji katika Vijiji kumi na Tano katika Wilaya hiyo.
Hivyo Mbunge huyo ameibana Serikali akiiitaka impe majibu ya kuridhisha kwani wananchi muda wote wamekuwa wakihoji.
Akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara ya Maji bungeni leo Machi 8,2025,Jijini Dodoma,Mbunge huyo amesema licha ya kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Maji lakini imeshindwa kutekeleza mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Tanganyika kwenda katika Wilaya hiyo mara baada ya wafadhili Wamarekani kujitoa.
"Na mimi natamani kufa hapa ili wana Nkasi wapate maji maana hili ni Bunge la mwisho, ni lini wana Nkasi watapata maji? Inawezekana ama la! Alihoji Mbunge huyo.
Kenan amesema upatikanaji wa maji safi Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa bado ni changamoto, ambapo mpaka sasa upatikanaji wake ni asilimia 49.
Amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo Serikali inatakiwa kutoa maji kutoka Ziwa Tanganyika jambo ambalo linahitaji dhamira ya dhati toka kwa watendaji.
Amesema Wilaya ya Nkasi ilibahatika kupata Miradi mitano katika Vijiji kumi na Tano ambapo amedai Miradi hiyo kwa sasa imesimama.
"Na wewe unafahamu, mtegemea cha ndugu, hufa masikini natamani utakapo kuja hapa Serikali ibebe mzigo huu, tunahitaji kupata 'commitment'ya Serikali kwa Wananchi kwani wana matumaini makubwa na hatuna jambo la kuwaeleza mara baada ya Marekani kujitoa,"amesema Mbunge huyo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...