Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye ameiongoza Menejimenti ya Mamlaka hiyo kupata mafunzo katika nyanja mbalimbali ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi kulingana na wakati.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu jijini Arusha kuanzia tarehe 5-7 Mei, 2025 yalijikita katika sheria ya maadili ya viongozi wa Umma, sifa za uongozi,  utunzaji wa siri na nyaraka za Serikali, uedeshaji wa ofisi za Umma, afya ya akili na akili hisia

“Mafunzo mahala pa kazi yanaimarisha utendaji kazi hasa katika utekelezaji wa majukumu, dunia inabadilika kwa sasa kuna masuala ya akili hisia “emotional intelligence”, akili mnemba “artificial intelligence”, maadili katika utumishi wa Umma, uendeshaji wa ofisi za umma na kuongeza ufanisi katika kuhudumia wateja wetu, sasa ili kuongeza ufanisi katika masuala haya tuna wajibu wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara ambayo pia yatatusaidia  kuongoza tunaowasimamia ”  alisisitiza Dkt. Doriye. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...