Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ludewa Shukrani Kawogo amewataka wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani humo kujitokeza katika Matawi na kuchukua Kadi zao za Kielektroniki kupitia makatibu Tawi waliko jisajilia.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mwenezi huyo amesema kuwa CCM wilayani humo kimepokea Kadi za Kielektroniki zipatazo Elfu 48 na zinatarajiwa kuanza kugawiwa Mei 22 mwaka huu.

" Ludewa hatuna jambo dogo hivyo suala hili la kugawa Kadi kwetu ni kubwa na tutahakikisha wilaya yote itazizima kwa shughuli zinazoendelea matawini".

Sanjali na hilo pia amesisitiza kuwa Kadi hizo hutolewa bure pasipo malipo ya aina yoyote bali mwanachama anachotakiwa kwenda nacho ni kitambulisho cha Nida sambamba na kitambulisho cha Mpiga kura ili kuweza kuhakiki taarifa zilizopo kwenye vitambulisho hivyo na Kadi ya uanachama.

Aidha ameongeza kuwa zoezi hili linawahusu wanachama wote waliosajiliwa katika mfumo bila kujali kama awali alipata Kadi ya Kielektroniki kwani Kadi za sasa zimeboreshwa hivyo wote watapatiwa upya.

" Kuna wale wanachama ambao miaka ya nyuma walipata Kadi za Kielektroniki, katika zoezi hili la sasa nao pia ni walengwa kwani Kadi za sasa zimeborezwa zaidi ukilinganisha na zile za wali hivyo nao wafike ili waweze kupatiwa Kadi mpya".







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...