VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya picha ya ndege Grace Jungulu amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwemo kutenga fedha nyingi ambazo zimekwenda kuwa mkombozi kwa wananchi katika suala zima la utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.

Jungulu ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusiana na mafanikio mbali mbali ambayo yametekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu hassan kwa kipindi chake cha miaka minne ambapo ameweza kufanya mambo makubwa ya kimabadiliko kwa kuwaletea chachu ya wananchi ikiwemo kuwawezesha kiuchumi kwa kupitia fursa za mikopo.

Pia Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kwa kipindi cha muda wa miaka minne kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo imeweza kutekelezwa katika nyanja mbali mbali ikiwemo miundombinu ya barabra, afya, elimu, maji, pamoja na huduma za kijamii kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wananchi.

"Kwa kweli Rais wetu wa awamu ya sitaDkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa sana katika ngazi mbali mbali za kuanzia miradi ya chini hadi ile mingine ya kimakakati lakini hata kwetu katika kata ya Picha ya ndege tunapenda sana kumshukuru kwani ametuletelea fedha nyingi ambazo zimeweza kutekeleza miradi mbali mbali ya ikiwemo afya, elimu, maji, pamoja na miundombinu ya barabara kwa hiyo tunampongeza sana Rais wetu,"amebainisha Mwenyekiti Jungulu.

Pia Jungulu ametumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe: Silvestry Koka kwa kuweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kutumia fedha a mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo hususan katika kuboresha elimu ha sa kwa shule ambazo zipo maeneo ya pembezoni.

Kadhalika amekishukuru chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji amabcho kimeweza kumpa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha utekeelzaji wa ilani unafanyika kwa kiwango cha ahali ya juu ikiwemo pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kukijenga na kukiimarisha chama katika ngazi mbali mbali.

Katika hatua nyingine amesema utekelezaji wa miradi mbali mbali amabyo imefanyika katika kipindi cha miaka minne katika Kata ya Picha ya ndege imeweza kuwasaidia kwa kiwango kiubwa wananchi wa maeneo hayo pamoja na maeneo mengine ya jirani kuweza kupata huduma kwa urahisi hususan kupata huduma ya matibabu katika hospitali ya Lulanzi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...