Na Pamela Mollel,Mwanza

Ndege Tausi ni miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyochangia ongezeko kubwa la watalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa kisiwa cha saa nane iliyopo jijini Mwanza

Tausi ni jamii ya ndege kama Kanga na pia kuna zaidi ya aina kumi zinazopatikana katika bara la Africa

Wamejizolea umaarufu mkubwa kwa muonekano wao hasa dume anayetajwa kuwa kivutio kukubwa katika hifadhi ya saa nane kutokana na rangi yake pamoja na mkia unaochanua

Afisa Uhifadhi Mkuu,Pellogy Marandu Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibu kwa niaba ya Mkuu wa Hifadhi,anasema ndege Tausi amekuwa kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali hasa wa ndani wanaofika kujionea vivutio katika hifadhi hiyo

Anasema kuwa Hifadhi hiyo ndio ya kwanza kwa kuja na mradi wa kuongeza ndege hao hifadhini ambapo ulianza mwaka 2018 ,walianza naTausi 15 hadi sasa wapo jumla ya Tausi 40

"Jitihada za hifadhi ni kuhakikisha tunawalinda tumetenga eneo maalumu (cage )ili kukabiliana na changamoto yaPaka pori pamoja na nyoka"Anasema Marandu

Mwongozo Watalii katika hifadhi hiyo Iddy Ibrahim anasema kuwa watalii wa ndani wanavutiwa zaidi kumuona ndege tausi dume hasa pale anapochanua mkia wake uliopambwa na rangi nzuri za kuvutia

Ameongeza kuwa maajabu ya Tausi dume ndiye anayevutia na kumshawishi jike ambapo jike anauwezo wa kukutana na madume wengi zaidi

"Ndege hawa wanapendelea zaidi sehemu zenye joto wanauwezo wa kulalia mayai kwa siku 28 hadi 30"Anasema Ibrahim

Aidha ameongeza kuwa wanaweza kuishi kwanzia miaka 15 had 20 lakini pia wanakabiliwa zaidi na ugonjwa wa kideri.

Ndege Tausi anaheshima ya kipekee katika baadhi ya mataifa hapa duniani




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...