Pamela Mollel, Arusha.

Benki ya NMB imenunua na kugawa vitanda, madawati, viti na meza vyenye thamani ya Shilingi milioni 125.2 katika shule 15 za Wilaya ya Arusha na Arumeru.

Kati ya shule hizo zilizonufaika, 11 ni za Arusha Jiji ikiwemo shule za msingi Unga limited waliopewa madawati 150, huku Baraa, Lemara, Sanawari, Elerai na kijenge kila moja madawati 100.

Shule zingine ni za sekondari ambazo ni Ungalimited, Elerai, Kimaseki, Osunyai na Salei waliopewa viti na meza 50 kila mmoja.

Katika Wilaya ya Arumeru, shule ya Sekondari Oldadai imekabidhiwa vitanda (double decker) 33 huku Kiutu na Kiserian wakikabidhiwa viti na meza 60 kila moja na shule ya msingi Mussa ikipewa madawati 50.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa NMB Kanda ya kaskazini, Baraka Ladislaus amesema vifaa hivyo vina thamani ya Shilingi milioni 125.2

"Kwa shule za Arusha Jiji vifaa vyao vina thamani ya Shilingi milioni 88.2 huku Arumeru vikiwa na thamani ya Milioni 37";

" Lengo la kusaidia shule hizo ni kuhakikisha tunashirikiana na serikali katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii yetu hususani kwenye masuala ya Elimu na Afya" amesema Baraka.

Amesema kuwa wanatambua juhudi mbalimbali za makusudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta hizo ndio maana wamekuwa mstari mbele kusaidia.

"Kukabidhi vifaa hivi leo ni kuthibitisha moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama Benki inayoongoza Tanzania, tunao wajibu wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata"

Amesema kwa miaka 10 mfululizo wamekuwa tukitenga asilimia moja ya faida kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotunzunguka.

"Juhudi zetu hizi za kusaidia jamii tumeweza kutambulika na Jarida la Global Banking & Finance Magazine lenye makao yake New Jersey, Marekani kama Kinara wa Uwajibikaji kwa Jamii Tanzania 2025 vilevile kututambua kwa ubora wa huduma zetu kama Benki Salama Zaidi Nchini Tanzania".

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha , Joseph Mkude ameipongeza benki ya NMB kwa kubaini changamoto mbalimbali za kwenye jamii na kusaidia.

Pia ameitaka uongozi wa shule na bodi zake kuhakikisha vifaa hivyo vinalindwa Ili ziweze kuwa msaada kwa wanafunzi wa sasa na baadae wanaokuja.

Nae mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Amri Mkalipa ameishukuru NMB kwa msaada huo wa viti na kuwataka walimu wa shule zote kuhakikisha wanaunda kamati za kuhakikisha miundombinu na vifaa vya shule vinalindwa.

"Kuanzia sasa hivi watoto wakorofi wanaoharibu miundombinu na vifaa vya shule hasa viti na meza kwa makusudi, wazazi waandikiwe barua walipe Ili kupunguza changamoto ndogo ndogo za uhaba wa viti na meza kila mwaka wakati serikali na wadau wanaleta" amesema.
Meneja wa NMB Kanda ya kaskazini Baraka Ladislaus akikabidhi sehemu ya vitanda 33 kwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amri Mkalipa



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...