
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Medali ya Mother of the Nation Order kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan. Medali hiyo iliwasilishwa kwake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.
Aidha, Medali hiyo ni moja kati ya Medali za juu kabisa kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Medali hiyo hutolewa kutambua mchango Kiongozi katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yake. Serikali ya UAE imetambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu ambayo yanaendana na Sera za UAE za maendeleo endelevu katika kijamii, uwezeshaji wanawake na ushirikiano wa kimataifa.
Sheikh Abdullah aliwasilisha salamu kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na kuwatakia kheri wananchi wa Tanzania katika maendeleo pamoja na ustawi zaidi. Pia alisisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa kudumu baina ya nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa kupanua ushirikiano katika sekta muhimu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...