Na Oscar Assenga,TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amesema kwamba takwimu ni nguzo na nyenzo muhimu katika kupanda utekelezaji wa mipango mbalimbali maendeleo duniani.

Dkt Batilda aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS) ambapo alisema kwamba mabazara hayo yana maada mkubwa kwa wafanyakazi.



Ambapo alisema kwamba Serikali inatambua jukumu hilo kubwa la (NBS) kuzalisha na kusambaza pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa takwimu rasmi kwa ajili ya kupanda utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika nchi.

Alisema kutokana na hilo wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa utashi wake mkubwa wa kisiasa alionao katika kuendeleza Tasnia ya Takwimu nchini na wote wameona mafanikio yake .



“Wote tunaona kwa namna ya kipekee Serikali ya awamu ya sita imekuwa mstari wa mbele kuwezesha uzalishaji wa takwimu rasmi pamoja na matumizi ya takwimu katika mipango mbalimbali ya maendeleo na Dira bila takwimu hakuna kinachoendelea”Alisema



Hata hivyo aliipongeza timu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa umoja na mshikamano kutokana na takwimu huanzia katika uzalishaji,uchakataji wake,uhakiki wake mpaka usambazaji wake kutokana na kwamba mtu moja hawezi kufanya pekee yake hivyo lazima wafanye kazi kwa ushirikiano.



Alisema kwamba wanaendelea kuhamasisha wenzao wajiunge kwebye vyama vya wafan yakazi hasa tughe ili waweze na kauli kubwa ambavyo itakuwa na maslahi mapana kwa nchi na sisi wenyewe.



Aidha aliwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa tija na uzalendo na kuongea nao waelewe dira na dhima ya taasisi zao na mambo ambayo hawataji kuyaona kwenye taasisi zao ikiwemo uvujaji wa siri.

“Katika mambo ambayo tunawapongeza sana NBS ni usiri mkubwa mlionao kwa kweli mnafanya kazi kubwa na sasa wanakwenda kwenye teknolojia ya habari tunaweza kuwa na usiri lakini mkaingiliwa kuna viti ya kimtandao inabidi tuendelee kujiimarisha sana kwa maana nyie ndio wamebeba roho ya nchi”Alisema



Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sababu taarifa zote zipo kwao kwa hiyo wajipange na moja ya maeneo ambayo watapaleka watu wengi kusoma ni masuala ya ulinzi wa kimtandao ili kuungana na kikosi kazi cha Serikali ili kuhakikisha kwamba taarifa zinakuwa salama na hakuna jambo ambalo litaingizwa.



Awali akizungumza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (NBS) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Amina Msengwa alimshukru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kumteua kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali anatambua heshima kubwa aliyopewa na kuhaidi kuendelea kusimamia ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa maelekezo na waledi mkubwa ili kuhakikisha majukumu ya NBS yanakwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya Rais.



“Nimshukuru Kamisaa Anna Makinda kwa kuendelea kutusaidia katika ushauri lakini kusimamia mkakati wetu wa usambazaji wa matokeo ya Sensa na tunaendelea kujivunia kutoka kwake”Alisema

Aidha alisema kwamba kupitia ofisi ya Taifa ya Takwimu wanataka kuijenga Tanzania yenye maendeleo ya juu kabisa huku akieleza kwamba wamekuwa wakitekeleza sheria na kanuni za zinazoongoza uundaaji na uendeshaji na u vikao vya mabaraza la wafanyakazi .



Naye kwa upande wake Kamisa wa Sensa na Spika wa Bunge Mstaafu Anna Makinda alisema baraza la wafanyakazi ndio roho muhimu ambayo inaunganisha wafanyakazi na menejimenti ambapo alitumia wasaa huo kuwataka watumishi kujiunga kwenye mabaraza hayo kutokana na uwepo wa manufaa mbalimbali.

Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...