Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 

HATIMAE wanafunzi watatu wa kike kutoka vyuo vikuu mbalimbali Jijini Dar es Salaam wanaodaiwa kumdhalilisha mwenzao mitandaoni, wamefikishwa katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka nane, ikiwemo kula njama na kutishia kumuua mwenzao Magnificat Kimaro kwa kisu

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Tumaini Mafuru imewataja washtakiwa hao kuwa ni Mary Matogoro (22) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Mkazi wa Sinza, Ryner Mkwawili (22), Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi, Dar es Salaam Mkazi wa Makongo na Asha Juma (22), Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam Mkazi wa Kigamboni.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga inadaiwa Machi 16, 2025, katika eneo la Sinza, Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es salaam washtakiwa walikula njama ya kuchapisha taarifa za uongo.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la pili Matogoro na Juma wanatuhumiwa Machi, 2025 wakiwa katika eneo lisilofahamika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walichapisha taarifa za uongo zilizosomeka, 'Toa sauti umefuck na mpenzi wa Mwijaku lini, umefuck nae wapi'? kwa lengo la kumkashifu  Magnificat Kimario.

Taarifa hiyo ilikuwa katika mfumo wa kumpyuta na kusambaza katika mtandao wa WhatsApp na kumshakishifu hadharani Kimario huku wakifahamu taarifa hizo ni za uongo. 

Ilidaiwa Machi 16,2025 Matogoro akiwa eneo la Sinza alimshambulia Kimario kichwani kwa kutumia chuma, na kumsababishia madhara makubwa sehemu zake za kichwani.

Pia, katika shtaka la tano washtakiwa wanatuhumiwa kumsababishia madhara makubwa Kimario kwa kumvuta nywele zake kwa kutumia nguvu. Matogoro anatuhumiwa bila uhalali wowote aliharibu laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina Magnificat Kimario.

Katika shtaka la saba, Matogoro anatuhumiwa Machi 16,2025 akiwa eneo la Sinza bila kuwa na uhalali aliharibu simu moja yenye thamani ya Sh 700,000 mali ya Kimario. Shtaka la nane washtakiwa wanatuhumiwa kumtishia kumuua Kimario kwa kutumia kisu.

 Hata hivyo washtakiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na mpaka muda wa mahakama unaisha mshtakiwa Mary alikuwa hajafanikiwa kutimiza masharti ya dhamana huku wenzie wakiwa wamefanikiwa.

Katika masharti hayo, mahakama imewataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya NIDA pamoja na barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi bado unaendelea, na kesi imeahirishwa hadi Juni 13, 2025 itakapokuja  kwa ajili ya kutajwa.

Ikumbukwe kuwa taarifa ya Jeshi la Polisi ya Aprili 24, 2025, ilidai wanafunzi hao walihojiwa kuhusiana na tuhuma hizo na walithibitisha kumuhoji Mwemba Burton Mwemba, maarufu kama Mwijaku, kuhusu kesi hiyo kutokana na video iliyosambaa Aprili 20,2025 katika mitandao kijamii ikionesha washtakiwa wakigombana huku wakimuhusisha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwijaku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...