Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Halmashauri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) imemteua wanachama watatu waliojiunga na Chama hicho ambao wametokea Chadema kushika nafasi za juu,  Salum Mwalimu   kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho  Mwalimu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mohammed Masoud Rashid, ambaye ametangaza kuachia ngazi muda mfupi uliopita.

Mwengine aliyeteuliwa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Devotta Minja kuwa kaimu makamu mwenyekiti. Devotta ameteuliwa leo Jumatatu, Mei 19, 2025 muda mfupi baada ya kutambuliwa na kupewa kadi ya uanachama ndani ya Chaumma.

Halmashauri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) pa imemteua Benson Kigaila kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara. Kigaila ambaye alikuwa akiunda kundi la G55 lililoanzisha harakati na kwenda kinyume na uongozi wa sasa wa Chadema, ametangazwa leo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chaumma kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu Mei 19, 2025.

Mambo yameanza kuchangamka ndani ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), baada ya viongozi watatu wa kitaifa kujiuzulu nafasi zao, wakitaja sababu ni kukipa chama hicho fursa ya kuwapata viongozi wengine watakaoendeleza gurudumu mbele.

Waliotangaza kujiuzulu ni Katibu Mkuu wa chama hicho Mohammed Masoud Rashid, Naibu Katibu Mkuu Bara, Rahman Rungwe na Makamu Mwenyekiti Bara, Kayungo Mohammed.

Hata hivyo, uamuzi wa kujiengua kwao unahusishwa na kuwapisha viongozi wapya watakaotokana na wanachama wapya watakaopokelewa leo wakiwamo waliojivua uanachama wa Chadema.

Akitoka taarifa ya kujiuzulu kwake mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Chaumma leo, Jumatatu Mei 19, 2025 Katibu Mkuu wa chama hicho, Mohammed Masoud Rashid amesema ameachia ngazi kwa manufaa ya chama chake.

"Kwa sababu tunakiongoza chama na kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 53 nimeamua kujiuzulu ukatibu mkuu kwa madhumuni ya kukifanya chama changu na halmashauri kuu kazi yake kubwa ni kutafuta wanachama, kuingiza wanachama na wawe wanaweza kukubalika kwa wananchi.”

“Nimeachia ngazi kwa sababu ya manufaa ya chama changu ili tuongeze wanachama wengine watakaoleta manufaa kwa wananchi wetu. Sio haramu ni halali kabisa," amesema.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...