Serikali imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na waandaaji wa Tuzo za muziki wa injili Afrika Mashariki East Africa Gospel Awards,(EAGMA) ili kusaidia kufika mbali zaidi katika kuhakikisha vipaji vya wanamziki vinazidi kukua.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Kalman Mapena wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo.
Mapena amesema tuzo hizo ni za kihistoria kwa sababu zinafanyika kwa mara ya kwanza hivyo ni vema kuhakikisha zinasimamiwa kikamilifu katika kuhakikisha zinakuwa endelevu.
“Mawazo yenu yawe ya muda mrefu yanayotekelezeka na yanadumu,kumuimbia Mungu ni kusali mara mbili, hivyo waliojitolea kumuimbia Mungu wanatusaidia kusali mara mbili,”amesema
Amesema wazo hili la uwepo wa Tuzo hizo lisiangalie tu kwa nchi za Afrika Mashariki pekee ila liende mbali zaidi kwa nchi zote za Afrika.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania, Ado November, amesema kuwa Tanzania imeshirikiana na East Africa Gospel Awards,(EAGMA) zikihusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, na Sudani Kusini.
Ado November ameongeza kuwa tuzo hizo zitakuwa faraja kwa wasanii wa muziki wa Injili nchini Tanzania, kwani jitihada zao za muda mrefu sasa zinakwenda kuleta matunda.
“Muziki huu sasa utwafuta machozi wasanii wetu baada ya kuufanya kwa muda mrefu, lengo la tuzo hizi ni kuwaleta pamoja wanamuziki wa injili ambao wanafanyakazi kubwa katika kuelimisha na kuburudisha jamii yetu kwa ujumla,” alisema.
Aidha amesema tuzo hizo zinatarajiwa kuinua na kuthamini mchango wa wasanii wa Injili katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku zikitoa jukwaa la kuutangaza muziki wao kimataifa.
Kwa upande wake Muandaaji wa Tuzo hizo EAGMA,Magreth Chacha amesema EAGMA inaunganisha wasanii,mashabiti na wataalamu wa sekta ya muziki kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Amesema madhumuni ya muanzisha tuzo hizi ni pamoja na kuvuna nafsi kwa kristo kupitia nguvu ya muziki wa injili hasa kwa vijana ambao mara nyingi wanapotea kwenda kuimba muziki wa kidunia.
“Tunajitahidi kutengeneza muziki wa kuleta mabadiliko ya kudumu katika kusherehekea vipaji vya muziki wa dini.
“Tukio hili la Tuzo za Injili kwa nchi za Afrika Mashariki ni tukio la matumaini hamasa na imani zinazokutana katika kusherehekea nguvu za muziki wa injili,”amesema.

Katibu Mtendaji wa Baraza Sanaa la Taifa (BASATA), Dk. Kelman Mapena (wa kushoto), Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado November (kushoto),Mkurugenzi Mtendaji (EAGMA), Magreth Chacha (wa pili kulia) na Ofisa kutoka Ofisi ya Haki Miliki Tanzania, (COSOTA), Anitha Jonas, wakionyesha moja kati ya Tuzo zitakawaniwa katika tuzo za njimbo za Injili Afrka Mashariki, itakayofanyika hivi karibuni wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Katibu Mtendaji wa Baraza Sanaa la Taifa (BASATA), Dk. Kelman Mapena (kushoto)(kushoto),Mkurugenzi Mtendaji EAGMA,muandaaji wa Tamasha la nyombo za Injili Afrika Mashariki, Magreth Chacha (wa pili kulia) na Ofisa kutoka Ofisi ya Haki Miliki Tanzania, (COSOTA), Anitha Jonas,wakicheza muziki wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...