NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

BENKI ya Standard Chartered imepanda miche ya miti 2000 katika shule ya msingi Fukayose iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuhamasisha ulinzi wa mazingira.

Akizungumza Mei 17,2025 wilayani Bagamoyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Majid Mhina ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo katika zoezi hilo alisema kiwango cha uzalishaji wa hewa ukaa ni kikubwa kuliko idadi ya miti, jambo linalochangia kuongezeka kwa magonjwa na uhaba wa chakula.

Aidha Mhina aliwasihi wadau kuongeza juhudi za upandaji miti kwa ajili ya kurejesha mvua na kuongeza uzalishaji wa chakula.

Pamoja na hayo Mhina aliipongeza Standard Chartered kwa kujitolea kwake bila kuyumbayumba kwenye uendelevu wa mazingira kupitia mpango wake wa upandaji miti,ikisisitiza upatanisho na malengo ya kitaifa ya hatua za hali ya hewa.

“Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa inayogusa uchumi, afya, na maisha ya wananchi wetu. Mipango kama hii siyo tu kwamba inarejesha uoto wa asili, bali pia inawafundisha vijana wetu umuhimu wa utunzaji wa mazingira,”

“Kwa ushirikiano baina ya serikali, sekta binafsi, na wananchi, tunaweza kufikia lengo letu la kitaifa la kupanda miti milioni 1.5 katika kila kata. Uongozi wa Standard Chartered katika suala hili ni mfano wa kuigwa katika uwajibikaji wa kampuni kwa jamii.” Alisema

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu Standard Chartered Herman Kasekende, alieleza kuwa zoezi hilo wanalolifanya ni muhimu kwani litasaidia kupunguza hewa ukaa ambayo ni sumu mbaya.

"Wanasayansi wamefanya tafiti mbalimbali ambapo wanasema mti mkubwa unauwezo wa kufyonza karibu kilo 21.77 mpaka kilo 31.5 za hewa ukaa kwa mwaka, hivyo kuna umuhimu mkubwa tukaongeza jitihada za upandaji miti katika maeneo yetu"Alisema

Alisema katika benki yao wameweka mpango ambao umelenga ifikapo mwaka 2050 kufikia neti 0 (kupunguza hewa ukaa) kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo upandaji wa miti.

BENKI ya Standard Chartered,imefanya zoezi hilo katika shule ya msingi Fukayosi ambapo imekusudia kuwaandaa wanafunzi kudumisha usawa wa kiikolojia wa muda mrefu na kuongeza ufahamu wa mazingira kwa watoto,waalimu,na wanajamii ili kushiriki katika kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), hususan SDG 13 kuhusu hali ya hewa na SDG 15 juu ya maisha ardhini.




















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...