Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa of wa Dodoma Christopher Myava amesema katika utendaji kazi wa Takukuru mkoani humo katika kipindi cha Januari - Machi 2025 jumla ya shiningi milioni 13,555,000 zimeokolewa kutokana na ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya Maendelea 32 ya sekta ya elimu afya, ujenzi, barabara na Maendelea ya jamii.
Mgava ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo ya robo tatu ya mwaka kuanzia Januari hadi Machi Mwaka huu 2025.
Amesema katika jitihada za kuzuia vitendo vya rushwa Takukuru inalo jukumu la kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Maendelea ili kuhakikisha kuaa miradi ya Maendelea inatekelezwa kwa ufanisi, lakini pia thamani ya Fedha katika miradi hiyo.
Taasisi hiyo ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini imeitaja sekta ya Ardhi kuwa kinara wa malalamiko yenye viashiria vya rushwa katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
Aidha Takukuru imewatahadharisha wagombea katika nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu kutojihusisha na vitendo vya rushwa ikiwemo kuwarubuni wananchi ili waweze kuwachagua kushika nyadhifa hizo.
Myava amesema Sekta ya Ardhi inaongoza kuwa na malalamiko 47 yenye viashiria vya Rushwa,ikifuatiwa na sekta ya elimu ikiwa na malalamiko 18,huku Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI),ikiwa na malalamiko 15, huku Polisi ikiwa na malalamiko 10.
Sekta nyingine Sekta binafsi ambayo ina malalamiko nane,ikifuatiwa na sekta ya Kilimo yenye malalamiko sita,huku Utawala na sekta ya maji na Afya zina malalamiko matano,ikifuatiwa na sekta ya Mifugo,Mahakama,Fedha na serikali Kuu zina malalamiko manne.
Sekta nyingine ni Madini ambayo ina malalamiko matatu huku Nishati ikiwa haina malalamiko yoyote yale yenye viashiria vya rushwa.
Akizungumzia kuhusiana na suala la kuelekea uchaguzi Mkuu,Myava amewatahadhalisha wagombea na nafasi mbalimbali za uchaguzi Mkuu kutojihusisha na vitendo vya rushwa badala yake wafuate taratibu za uchaguzi zinavyoelekezwa.
Amesema wao kama Takukuru wamejipanga kuhakikisha wanakabiliana na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu hapa nchini.
"Nawasihi wananchi msikubali kurubuniwa na wagombea kuelekea uchaguzi mkuu Takukuru itaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali kuhusu masuala ya rushwa,"alisema Myava.
Alisema katika sekta ya Elimu,Afya na Ujenzi wa barabara sh milioni tisa zililipwa kwa Mzabuni kwa matofali ambayo yalikuwa chini ya kiwango ya mradi wa ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Kalenga na sh milioni tatu fedha zilizidishwa katika malipo ya ununuzi wa madirisha ya Aluminium ya shule ya sekondari ya Manchali.
Hata hivyo amesema kikao kilichofanyika na Mzabuni kilibaini kuwa matofali hayo yalikuwa na kiwango cha chini na kurejesha kiasi hiko cha fedha pamoja na kile cha mzabuni wa mradi wa ujenzi wa madirisha.
Kutokana na hilo.aliwatka wazabuni wanaokabidhiwa miradi kuitelekeleza kwa ufasaha kulingana na fedha halisi inayotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo mkoani humo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...