Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na Nchi Wanachama wa Mkataba wa Lusaka katika kukabiliana na biashara haramu ya Wanyamapori na mazao ya misitu inayovuka mipaka ya Nchi ili kuboresha uhifadhi, kuendeleza utalii na kukuza uchumi.
Akifungua Mkutano wa 14 wa Kamati ya Wataalam wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka ulioanza Mei 06, 2025 Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Wanyamapori Dkt. Alexander Lobora amesema Mkataba huo umekuwa na manufaa makubwa kwa Nchi Wanachama kwa kuunganisha nguvu za pamoja kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.
“Tumekuwa tukishirikiana na nchi nyingine kwa kupeana taarifa za kiintelijesia za wahalifu pale ambapo wanatenda kosa na kukimbilia nchi nyingine, au kuwa na washirika wa uhalifu katika mataifa mengine na kuchukua hatua za kuwakamata na kuwarudisha katika nchi walikotenda uhalifu ili sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.” Amesema Dkt. Lobora
Aidha Dkt. Lobora amesisitiza juu ya wananchi wanaojishughulisha na ujangili kuacha mara moja na kujielekeza katika kazi halali za kujipatia kipato kwa kuwa utekezaji wa mkataba huo hautaruhusu wahalifu kujificha popote.
Awali, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Huduma za Wanyamapori Kenya Prof. Erustus Kanga ametoa rai kwa nchi za Afrika kushirikiana katika juhudi za kupambana na biashara haramu za mazao wanyamapori na misitu ikiwemo uwindaji haramu wa wa wanyamapori adimu wakiwemo faru kwa ajili ya vipusa na ndovu kwa ajili ya meno yao.
“Kupitia mkaba huu tungependa kuona Bara letu la Afrika hakuna mtu yeyote anayejihusisha na uwindaji haramu, wa Faru au Ndovu, atoe pembe Kenya ama atoe Tanzania na avuke mipaka ama, atoke Tanzania aende Zambia ama atoke Kenya aende kuziuza Kongo, hilo ndiyo jawabu letu kubwa kabisa. Tunataka kuona rasilimali zetu zinalindwa kwa kukomesha biashara haramu za mazao ya wanyamapori na misitu ili tuweze kunufaika na rasilimali zetu za asili.” Amesema Prof. Kanga
Mkataba wa Lusaka ulianzishwa mwaka 1994 Jijini Lusaka Zambia na Tanzania ni miongoni mwa mataifa sita yaliyoanzisha Mkataba na kuridhia utekelezaji wake mwaka 1996. Katika Mkutano wa 14 wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba, Tanzania itakadhiwa kiti cha urais wa Baraza kwa kipindi cha miaka miwili kutoka Kenya.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...