SERIKALI ya Tanzania imeendelea kupata pongezi kutoka kwa wawekezaji wa kigeni kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya biashara, ikiwemo kurahisisha taratibu za usajili wa kampuni na kuwapa wawekezaji fursa ya kuanza shughuli haraka bila vikwazo vikubwa vya kiutendaji.


 Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni ya Teknolojia ya Spidd Africa nchini, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Catherine Kisaka, amesema Tanzania imeonesha dhamira ya dhati ya kuvutia wawekezaji kupitia sheria rafiki na mifumo ya kidijitali inayowezesha usajili wa haraka wa kampuni.


Ameeleza kwamba Spidd Africa, kampuni yenye makao makuu nchini Uganda, inalenga kuleta mageuzi ya kidijitali katika sekta ya biashara barani Afrika kupitia suluhisho bunifu, hususani kwa wajasiriamali wadogo, biashara za kati, na mashirika makubwa.


Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Spidd Afrika kutoka Uganda, Angela Semwogerere, amebainisha kwamba moja ya malengo makuu ya kampuni hiyo ni kutoa elimu na mafunzo kuhusu usalama wa kimtandao kwa taasisi mbalimbali, ili kuongeza uelewa na ulinzi wa taarifa katika ulimwengu wa kidijitali.

Kufunguliwa kwa tawi la Spidd Africa nchini kunatarajiwa kuchochea mabadiliko chanya katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, pamoja na kukuza ajira na ubunifu kwa vijana wa Kitanzania.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...