Na Janeth Raphael
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF),umelenga kuwanusuru walengwa wanaotoka katika Kaya maskini kwa kuwapatia kiasi cha fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi wao na familia zao katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Fedha hizo zimekuwa msaada mkubwa sana kwa baadhi ya kaya za walengwa wanaopokea kwa ajili ya kujikimu lakini pia wengine wanajiongeza kupitia mgao huo,wanabuni kufanya biashara ndogo ndogo za vyakula,wengine ufugaji pamoja na kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na eneo analoishi.
Serikali kupitia TASAF imekuwa ikitoa fedha hizo kwa walengwa kupitia halmashauri zake ambazo huwa na idadi ya Kaya za walengwa ambao wanakidhi vigezo vya kuingia kwenye mpango wa kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na serikali katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
TASAF awamu ya tatu,kipindi cha pili cha Mpango wa kunusuru Kaya maskini kikiwa kinaelekea mwishoni ili kuingia kipindi kingine cha mpango huo,imetembelea miradi iliokuwa ikitekelezwa pamoja na kuwatembelea walengwa wake ili kujionea nini wanafanya kupitia fedha hizo zinazotolewa na serikali kwa walengwa wa Kaya hizo.
Katika ziara yake TASAF walitembelea halmashauri za wilaya za mkoa wa Dodoma kukagua miradi walioitekeleza,lakini pia kukutana na walengwa ambao wananufaika na mpango huo wa kunusuru kaya maskini.
Halmashauri walizopita ni pamoja na halmashauri ya Kondoa,Chamwino,Chemba,Kongwa,na Mpwapwa,ambako kote huko walikagua miradi pamoja na kuwatembelea wanufaika wa mango ikiwemo kuzungumza nao ikiwemo kuona shughuli wanazofanya kwa ajili ya kujiongezea kipato.
MAHOJIANO NA WALENGWA WA TASAF
Christina Fwande mkazi wa kijiji cha Gawaye kilichopo wilaya ya Dodoma mjini mkoani hapa anasema ameanza kuchukua fedha za mfuko wa maendeleo ya Jamii nchini TASAF, zinazotolewa kwa walengwa wanaotoka kwenye Kaya maskini akiwa na hali duni ya maisha kwenye familia yake.
Fwande anasema alianza kupokea sh kiasi kulingana na idadi ya walengwa waliopo,lakini fedha ile akawa anaigawanya kwenye matumizi vyakula vya nyumbani huku nyingine akiitunza Kwa kuchangisha kila anapopata mgao huo.
Anafafanua zaidi ya kuwa,baada ya kufikia kiasi kadhaa cha fedha,alinunua ng'ombe mmoja,pamoja na jembe la kulimia (Plau),kwa ajili ya kulimia kwenye mashamba yake ikiwemo kukodisha ng'ombe hao kwa wanakijiji wengine pindi msimu wa kilimo unapowadia.
"Ng'ombe wawili na jembe hilo la kulimia nililonunua vilinisaidia sana kujiinua kiuchumi mimi na familia yangu huku nikiendelea kuwekeza fedha za walengwa ili zinisaidie kuendeleza familia yangu," anasema Fwande.
Fwande anasema alifanya zoezi hilo la utunzaji fedha kwa muda wa miezi kadhaa,akaongeza kununua ng'ombe wengine watatu na kufikia kuwa na idadi ya ng'ombe watano ambao wanamsaidia kuongeza kipato chake kutokana na kuzikodisha ng'ombe hizo kipindi cha msimu wa kilimo,lakini anakamua maziwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na machache huyauza kwa majirani.
"Ninaishkuru sana serikali kupitia TASAF kwa kutupatia fedha hizi walengwa tunaotoka kaya maskini,zimesaidia Kaya nyingi kujiinua kiuchumi na kuhitimu kupata fedha hizo ili kuzia hia kaya nyingine Amazon zinakidhi kuingia katika Mpango wa kunusuru Kaya maskini,"anasema Fwande.
KUHUSU MAFANIKIO ALIYOPATA KUPITIA FEDHA ZA TASAF
Christina Fwande anasema moja ya mafanikio aliyoyapata ni pamoja na kujenga nyumba ya kuishi aliyoiezeka kwa bati na kutoka kwenye nyumba ya tembe aliyokuwa anaishi awali kabla ya kuingia katika mpango wa kunusuru kaya maskini,kanunua mifugo zikiwemo ng'ombe,kuku Bata ambazo huzifuga,amesomesha watoto ambao bado wanaendelea na masomo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...