KUELEKEA Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maziwa mwaka huu, Bodi ya Maziwa nchini imeendelea kutoa wito kwa wananchi kuongeza unywaji wa maziwa, hasa yale yaliyosindikwa, ili kuboresha afya, lishe bora na kuunga mkono sekta ya maziwa nchini.
Akizungumza na waandishi wahabari leo Mei20,2025 katika mafunzo yaliyotolewa jijini Dar es salaam, Kaimu Msajili Bodi ya maziwa Tanzania Deorinidei Mng’ong’o amesema maziwa yaliyosindikwa ni salama kwa matumizi ya binadamu, yanadumu kwa muda mrefu na yana viwango bora vya usafi na virutubisho, hivyo kuwa chaguo bora kwa jamii zote, mijini na vijijini.
“Tunapoelekea kilele cha Wiki ya Maziwa, tunawakumbusha wananchi kuwa kuchagua maziwa yaliyosindikwa si tu ni njia ya kulinda afya zao, bali pia ni kuunga mkono juhudi za wakulima na viwanda vya maziwa nchini,” alisema Kaimu Msajili wa Bodi hiyo.
Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa maziwa katika lishe, kuhamasisha matumizi yake, na kutoa fursa kwa wadau wa sekta hiyo kuonesha mafanikio na changamoto zinazowakabili.
Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro kuanzia mei 27 hadi juni mosi mwaka huu.
Bodi ya Maziwa imeandaa shughuli mbalimbali zitakazofanyika kuelekea na wakati wa kilele cha wiki hiyo, zikiwemo maonesho ya bidhaa za maziwa, midahalo ya kitaaluma, na kampeni za uelimishaji mashuleni na katika jamii kwa ujumla.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...