Tunduru-Ruvuma

Wananchi wa Wilaya ya Tunduru wametakiwa kuilinda na kuitunza miundombinu ya barabara kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na kuepuka kutupa taka ovyo, ili barabara hizo zidumu na ziwe na manufaa ya muda mrefu kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi, wakati wa uzinduzi rasmi wa barabara ya Nguzo Sita – Muungano – Camp David, yenye urefu wa mita 500 kwa kiwango cha lami. Mradi huo uko chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Tunduru.

“Tunawaomba wananchi muwe walinzi wa maendeleo haya barabara hii itahudumia wanafunzi, wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla. Tukitupa taka ovyo au kuharibu mifereji, tutarudisha nyuma jitihada hizi,” amesema Ussi.

Barabara hiyo ambayo imegharimu shilingi 234,902,000.00 inatekelezwa na mkandarasi M/S BR AND ASSOCIATES CONSTRUCTORS LIMITED, na ilianza kujengwa mwezi Desemba 2023, ikitarajiwa kukamilika Oktoba 2024. Meneja wa TARURA Wilaya ya Tunduru, Mhandisi Silvanus M. Ngonyani, amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya miji na vijiji.

Katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge pia amewakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi kwa amani na utulivu, huku akieleza kuwa mwaka huu ni mwaka muhimu wa kisiasa nchini. Ameongeza kuwa agizo la Rais ni kuhakikisha miji inajengwa kwa mpangilio na mazingira bora, kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...