Na. Julius Mtatiro
Tukio la Ajali ya Mgodi Mwakitolyo unaomilikiwa na Kikundi cha Wachimbaji cha "HAPA KAZI TU!", limetokea Jumamosi, 17 Mei 2025, na mimi kwa dhamana yangu ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga na timu za uokozi tulifika eneo la ajali mara moja muda huo huo.
Tumeshirikiana na wananchi kufanya maokozi ya uhakika, tumefanikiwa kuwaokoa watu 11 kifusini wakiwa hai, watu 6 tumewatoa wakiwa wamefariki. Mchakato wa uokoaji umefanywa na mashine za kisasa za migodini, tulikuwa na mashine zaidi ya 10 lakini zilihitajika mashine 4 tu kukamilisha zoezi lote - ndiyo maana mashine zingine tulizuia zisishuke eneo la chini la maokozi, ambapo mashine 4 zilikuwa zinaendelea na kazi.
Ukiwa pale eneo la ajali utaona tulihamisha kifusi chote kilichowaangukia watu na kukichambua kwa mashine na mikono, hakukuwa na mtu mwingine yeyote aliyebakia ndani ya kifusi, na zoezi la uokoaji lilifanyika wananchi wote wakiwa wanaangalia kwa sababu lile ni eneo la wazi na ni eneo pana ambalo zinaweza kuingia excavators hata 20 kwa wakati mmoja, siyo kwamba ni eneo finyu lisilo na nafasi.
Pia, na bahati nzuri, eneo la Mwakitolyo na Shinyanga halina mtu yeyote ambaye labda anakosekana "missing person", majirani, ndugu, jamaa, marafiki, wapangaji, wenye nyumba na familia zote za Mwakitolyo na Shinyanga, zinakiri kuwa watu waliokosekana ghafla walikuwa wale 6 waliofariki na wale 11 wanaotibiwa.
Kwa hiyo siyo tu kwamba tumekamilisha maokozi haya kwa uzito wa kipekee, lakini pia tumeongoza kufuatilia ikiwa kuna mtu hapatikani, watu wote wa eneo la ajali wameridhishwa kuwa hakuna mwenzao aliyebakia kwenye kifusi.
Lakini pia kama nilivyosema, kifusi chote kilitolewa eneo la ajali na kuhamishiwa upande mwingine kabisa na ndipo tukapata hao watu 17 kwa mchanganuo huo.
Kama hiyo haitoshi, hata majeruhi walioko hospitalini walitueleza waziwazi siku ya ajali kuwa wakati ajali inatokea mgodini kulikuwa na watu takribani 17. Sikiliza hii video iliyorekodiwa siku ya ajali kusikia majeruhi aliyekuwa na wenzake eneo la ajali akifafanua idadi ya watu waliokuwepo wakati wa ajali (wanajuana).
Naomba tupuuze taarifa zozote zinazoeleza eti kuna watu, wenzetu, wameachwa chini ya kifusi. Taarifa hizo siyo sahihi, ni potofu, zinalenga kuzua taharuki na zenye malengo yasiyo sahihi - tuzipuuze.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...