Na Mwandishi Wetu


Mkurugezi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Shadrack Mziray amelishukuru Shirika la Chakula Duniani kwa Niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa  Mchango wao  wanaoutoa wa kunusuru kaya Masikini.

Amesema Shirika hilo la Chakula lina mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo ya Wananchi hali inayowasaidia kujikomboa na umasikini na kufanya miradi ya maendeleo.

Mziray amezitoa pongezi wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu mpango mpya wa TASAF awamu ya Tatu unaotarajiwa kuaza Oktoba mwaka huu.

Amesema katika kikao hicho Shirika la Chakula Duniani limekubali kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mpango mpya wa kunusuru kaya masikini.

Mkurugezi WPF Tanzania Ronald Tranbahuy amesema shirika hilo limeridhishwa na muendelezo katika miradi na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Wakati awamu ya Pili ya  Mpango wa kunusuru kaya Masikini ukitarajia kumalizia  Septemba nakuaza kwa awamu ya Tatu  Oktoba mwaka huu .Wadau wa Maendeleo wamekua na ziara mbali mbali za tathimini ya kawaida  ya kuangalia Maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa TASAF.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...