Na Janeth Raphael MichuziTv - BUNGENI Dodoma
KATIKA mwaka wa fedha 2025/26, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepanga kutekeleza vipaumbele vitano ikiwemo kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji wa elimu na mafunzo.
Vipaumbele hivyo vimetajwa leo Mei 12,2025 bungeni na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Amevitaja vipaumbele vingine ni kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa mafunzo ya amali katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
Pia kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu.
Vilevile kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuimarisha uwezo wa nchi katika utafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuchangia upatikanaji wa maendeleo endelevu.
"Katika hili, juhudi zaidi zitatumika kupeleka vijana wa Kitanzania kusomea mambo ya sayansi ya nyuklia, mambo ya kompyuta na akili-unde kwenye vyuo bora vilivyo nje ya nchi,"amesema Prof Mkenda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...