Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Mohamed Said Dimwa amewaasa wanachama wa Chama hicho kuepuka makundi ya uhasama, uzandii wakisiasa na udhaifu katika maamuzi wakati wa kuelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 2025.

"Chama chetu cha CCM kimejiimarisha kwa kuwa na mikakati ya kisayansi na madhubuti ya kuhakikisha tunapata ushindi na kudumu dhidi ya hila na mbinu za wapinzani ambao lengo lao ni kuturudisha nyuma"amesema Dkt.Dimwa.

Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dkt.Dimwa amesema hayo alipokua mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa chama yanayoendelea katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Kwa Mfipa Mkoani Pwani yameanza Juni 6 hadi 12.

Dkt.Dimwa ameendelea kwa kusema kuwa anawakumbusha viongozi hao ambao wako kwenye mafunzo kuwa wanajukumu la kwenda kutoa maelekezo ya chama kwa watendaji ikiwa ni pamoja na Jumuiya zote za CCM sambamba na kutii miongozi na maagizo ya chama ,kusimamia utekelezaji kwa vitendo, kuheshimu vikao vya katiba na kujenga nidhamu binafsi sambamba na kutekeleza maamuzi yote ya chama.

"Nawaagiza nendeni mkaendeleze mpango wa kushuka hadi kwenye matawi ili kuongeza wanachama nankuhimiza uwajibikaji ulipaji wa ada za chama, kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya uchaguzi ujao utakaofanyika Oktoba 2025.

"Nawasisitiza nendeni mkaimarishe chama na jumuiya zake zote ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kazi wa kina kwq ufuatiliaji wa shughuli za chama na kutoa maelekezo ambayo mlahakikishe kuwa yanatekelezwa" amesema Dkt.Dimwa.

Dkt. Dimwa amesema kuwa viongozi hao ambao wako kwenye mafunzo wanatakiwa kuwa daraja la mawasiliano linalofikisha utekelezaji wa maagizo ya chama hadi ngazi ya chini.


"Urafiki wetu baina ya CCM na CPC umependelea kuimarika kwa kupitia misaada ya kifedha , kitaaluma na kiufundi ikiwa ni pamoja na kufadhili kwa ukarimu mafunzo kama haya kwa wanachama na viongozi wa CCM.

CPC imewakilishwa na Mkufunzi Yao Jianguo atashirikiana na Naibu Mkurugenzi wa Kituo Cha Mabadilishano ya Kimataifa CPC-CIE Xu Sujian pia watashirikiana na timu ya wawakilishi wa CPC nchini Tanzania

Aidha Dkt. Dimwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amemwagiza amwaeleze kuwa wakawe mabalozi wa matumaini , maendeleo na mshikamano kwa wananchi wote hasa katia kipindi hiki muhimu tunapokaribia uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

"Ndugu wana mafunzo nimejulishwa kuwa mtakuwa na ma 17 zilizochaguliwa kwa umakini mkubwa ili kuwajengea uwezo wa hali ya juu wa Uongozi kimkakati na kiitikadi nawakumbusha kuwa dhima kubwa ya mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wa kiutendaji wa chama kwa ajili ya zoezi kubwa la uchaguzi mkuu ujao.

Napenda kutoa shukran za dhati kwa Chama Cha Kikomunisti Cha nchini China CPC kwa kuendelea kudumisha udugu,ushirikiano wa kihistoria na mshikamano wa kweli baina ya vyama vyetu na mataifa yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...