Na Mwandishi Wetu,Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa wito kwa wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia katika mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hadi uchaguzi mkuu wa dola Oktoba 2025.
Hayo wakati akizungumza na Kikundi cha Wanawake wa Kikiristo na Maendeleo Zanzibar kanda ya Magharib ‘B’ huko Kiembesamaki Unguja.
Dkt.Dimwa, amesema CCM inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi.
Alisema maendeleo yaliyofikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi yamechangiwa na nguvu kazi ya Wanawake wanaosimamia kikamilifu masuala mbalimbali ya kisiasa na kimaendeleo.
“Natoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wana uwezo wa kuleza mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Dhamira ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha wanachama wote wanapata haki na fursa sawa katika kuimarisha demokrasia.”alisema Dkt.Dimwa.
Aidha, alieleza kuwa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, chama hicho kimeweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kwa njia mbalimbali, ikiwemo mafunzo ya uongozi, uwezeshaji kiuchumi, na kuhamasisha ushiriki wao katika siasa.
Alitoa mfano wa wanawake walioshiriki harakati za kupigania maslahi ya CCM toka wakati wa ASP na TANU ambapo aliwataja waasisi hao ambao ni Bibi Titi Mohamed,Bi.Johari Yussuf Akida na Bi.Mwanaidi Dai.
Katika hotuba yake, Dkt. Dimwa pia alizungumzia umuhimu wa kupinga vitendo vya ubaguzi wa kidini na kikabila, na kuahidi kuwa CCM itaendelea kusimamia haki na usawa kwa wanachama wake wote.
Alisema kuwa chama kinaendelea kudhibiti vitendo vya rushwa ili kuhakikisha kila mwanachama anapata haki anayostahiki kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya Chama hicho.
Alisisitiza umuhimu wa wananchi kulinda amani na utulivu uliopo nchini ili kuhakikisha uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka 2025 unafanyika katika hali ya amani.
Alisema CCM itapata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 uliofanywa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya awamu ya nane chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi.
Naye Mwenyekiti wa Kikundi hicho,Catherine Peter Nao alieleza kuwa wataendelea kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanawake mbalimbali nchini kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi nchini.
Catherine,aleleza kuwa wamejipanga kuhamisha na kutangaza maendeleo yaliyotekelezwa na serikali zote mbili ili wananchi waweze kujua kazi zinazofanywa na serikali iliyopo madarakani.
Caption.
Picha no.99 na 77- NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa,akizungumza na kikundi cha Wanawake wa Kikiristo na Maendeleo kanda ya Magharib “B”.
Picha no.44-Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, pamoja na Viongozi wa Kikundi cha Wanawake wa Kikiristo Zanzibar.Picha na Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...