Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina kwa wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

......

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) – Kanda ya Kaskazini, leo tarehe 21 Juni 2025, imeendesha semina kwa wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu, alieleza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wadau hao kuhusu umuhimu wa kuzingatia vigezo na masharti katika utoaji wa huduma za usambazaji na uuzaji wa LPG ili kuepuka madhara na kufungiwa leseni.

Pia aliwataka wasambazaji wakuu (superdealers) nao kujenga tabia ya kuwapatia elimu wauzaji (dealers) kuhusu masuala ya usalama.

Mhandisi. Long’idu alisema EWURA inaendelea kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ukilenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.

Mhandisi wa Petroli, Magreth Mwita, alitoa utaratibu wa kupata leseni ya kusambaza na kuuza LPG, na kuwasisitiza kuzingatia matakwa ya kisheria na ya kiufundi katika biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na mizani, lakiri na kuepuka uchakachuaji.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina kwa wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina kwa wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina kwa wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

Mhandisi wa Petroli Magreth Mwita,akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...