
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Zikiwa zimesalia siku 17 kwa Waandishi wa Habari Kujisajili katika Mfumo wa TAI-HABARI ili kuomba Ithibati na Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card), tayari waliokidhi vigenzo vilivyoanishwa Kisheria wameanza kupewa Vitambulisho hivyo.
Waandishi wa Habari wa kwanza kufika Ofisi za Bodi zilizopo Mtaa wa Jamhuri Jijini Dar es Salaam kuchukua vitambulisho vyao ni David Mayunga, Erasto Vedasto na Fredrick Mwantandi wote kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Wengine waliokabidhiwa vitambulisho vyao ni Mhariri wa gazeti la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar- Zanzibaleo Mwanajuma Hassan na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Taasisi ya Goshen Tanzania-goshenonlinetv Isaya Momba.

Mfumo huo uliofunguliwa rasmi Mei 19 mwaka huu, unatoa fursa kwa Wahariri, Waandishi wa Habari, Wapiga Picha, Watangazaji wa Radio na Televisheni, Waandishi wa Kujitegemea na Waandaaji wa Vipindi, waliokidhi vigezo vya Kitaaluma kujisali na kujaza taarifa zao kupitia kiunganishi cha https://taihabari.jab.go.tz ili kuomba Ithibati na Kitambulisho ambapo mwisho wa kujisajili ni Juni 21 mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Wakili Patrick Kipangula amewapongeza waandishi hao na kutoa wito kwa waandishi wengine kuutumia vema muda uliotolewa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...