Leo tarehe 10 Juni 2025 Kamati ya Pamoja ya Wataalamu ya Uimarishaji Mpaka wa Tanzania na Rwanda (JTC) imetembelea eneo la mto Kagera lililopo wilayani Ngara mkoa wa Kagera ikiwa ni sehemu ya mpaka wa kimataifa.Eneo hilo la mto Kagera lililotembelewa ni sehemu ya mpaka wa kimataifa unaotenganisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi maarufu kama mafiga matatu pamoja na eneo la RUSUMO.
Uamuzi wa kutembelea maeneo hayo mawili ni sehemu ya programu ya kikao cha JTC kinachoendelea katika mji wa Ngara mkoani Kigera.
Lengo la kutembelea mpaka huo ni kuwezesha JTC Kuandaa mpango kazi wa uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...