Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Enock Koola, ambaye ni msomi wa masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Miradi, amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo. Hatua hiyo inaashiria dhamira yake ya kuchangia kikamilifu maendeleo ya wananchi wa Vunjo kupitia nafasi ya uwakilishi bungeni.
Mbali na taaluma yake, Enock Koola pia ni mfanyabiashara na mdau wa maendeleo ya jamii ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na jamii katika miradi ya kijamii na kiuchumi.
Kupitia uzoefu na maono yake, anaamini anaweza kuleta mabadiliko chanya na maendeleo endelevu kwa wananchi wa Jimbo la Vunjo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...