NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
KATA ya Mabogini iliyopo katika Jimbo la Moshi vijijini Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro imepokea fedha Bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yalibainishwa jana na Diwani wa Kata hiyo anayemaliza muda wake, Dkt. Bibiana Massawe wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika kata hiyo kwa kipindi cha miaka mitano (2020/2025) kwa wananchi na viongozi wa chama cha Mapinduzi matawi pamoja na mabalozi katika mkutano wa hadhara uliofanyika ofisi za kata.
Alisema kuwa, kata hiyo imefanyiwa mambo makubwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kudai kuwa kwa sasa wananchi hao hawamdai chochote bali yeye ndio anaowadai katika boksi la kura Oktoba mwaka huu.
"Tangua kuanzishwa kwa kata yetu yenye jumla ya vijiji 8 na vitongoji 45 hatujawahi kupokea fedha nyingi za maendeleo kama kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita hivyo tunamshukuru sana Rais kwa kutujali na kutungulia kata yetu kwa miradi mingi na mikubwa" Alisema Diwani Bibiana.
Alisema kuwa, katika sekta ya Afya wamepokea Bilioni 2.146 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa zahanati ya mji mpya, ujenzi wa choo cha zahanati ya Mabogini.
Diwani huyo alisema kuwa, katika sekta ya Elimu walipokea Bilioni 1.762 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari kijiji cha Mtakuja, pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo, nyumba za walimu, vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari zilizopo katika kata hiyo.
Aliongeza kuwa, katika sekta ya miundombinu ya barabara kata hiyo ilipokea fedha Bilioni 9.467 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ukarabati barabara za kata hiyo pamoja na uwekaji wa mitaro ya maji ya mvua pamoja na baadhi ya barabara kuinuliwa juu kwa kiwango cha changarawe.
Kuhusu sekta ya maji, Diwani huyo alidai kuwa, walipokea fedha milioni 500 kwa ajili vya usambazaji maji katika vijiji vya Mtakuja na Mserekia.
Alidai kuwa, kata hiyo ilipokea pia fedha milioni 113 kwa ajili ya mikopo ya mikundi vya Wanawake, Vijana, watu wenye ulemavu ambapo jumla ya vikundi 20 vimeweza kunufaika na mikopo hiyo.
Mbalimbali naafanikio hayo, Diwani huyo alisema kuwa, kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara kuharibika kutokana na mvua za masika zilizonyesha hali ambayo imepelekea adha kubwa ya usafiri kwa wananchi.
Alisema kuwa, changamoto nyingine ni huduma ya umeme kutofika baadhi ya vitongoji ambavyo ni Kivulini, Nguvu kazi, Kibosho na Majengo pamoja na huduma za maji safi kutofika kwenye vitongoji vya Upareni, Kivulini, Chekereni, Nguvu kazi, Uru, Relini, Jitegemee, Umoja na Upendo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...