MBUNGE wa Viti Maalum,Neema Lugangira ameshauri Serikali ipunguze gharama ambazo zisizo za lazima katika bajeti yake.

Ushauri huo ameutoa leo Juni 17,2025,bungeni wakati alichangia mjadala wa bajeti Kuu ya Serikali.

"Nashauri serikali ione namna ya kufanya tathmini ya gharama zake zote ili iweze kuondoa gharama ambazo sio za lazima,”amesema na kuongeza

“Spika alishawahi kunisemea bungeni utakuta magari ya serikali yanaweza yakakaa yana nguruma hata saa nne hadi tano serikali inaingia gharama ya mafuta pasipo ulazima kwa hiyo niombe sana serikali ikafanya tathmini ya gharama zake za uendeshaji na iweze kuondoa,”amesema Mbunge huyo

Kuhusu mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali, Mbunge huyo alisema bado yanapata changamoto katika sheria ya kodi ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshindwa kutofautisha kati ya biashara na Ngo’s.

“TRA inatambua Ngo’s kama ni biashara jambo ambalo linaleta changamoto kubwa na mkanganyiko mkubwa kwa hiyo niombe sana serikali kwa kutambua kwamba tayari Tanzania imepata mtikisiko ambao serikali inajitahidi kuhimili kufuatia mabadiliko ya fedha za wahisani, ni muhimu sasa sheria ya kodi ibadilishwe ili itofautishe kati ya Ngo’s na biashara,”amesema Mbunge huyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...