Na Said Mwishehe

MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika tamasha la nyama choma ambalo limefanyika katika soko la Kumbilamoto lililopo Vingunguti.

Lengo la tamasha hilo lilikuwa ni kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango na jitihada zake katika kuwawezesha wajasiriamali nchini kufanya shughuli zao katika mazingira mazuri kama yaliyopo katika Soko la Kumbilamoto ambalo ni maalum kwa nyama choma.

Akizungumza wakati wa tamasha la Nyama Choma kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia,Meya wa Dar es Salaam na Diwani Kata ya Vongunguti Omari Kumbilamoto amesema wanamshukuru Rais kwa kufanikisha ujenzi wa soko hilo ambalo limegharimu zaidi ya Sh.milioni 725.

“Tumeandaa tamasha hili kwa lengo maalum la kumpongeza na kumshukuru RaisDk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha wajasiriamali wetu kwa kuwajengea soko hilo la nyama choma. Leo hii wajasiriamali wananufaika na uwepo wa soko hili na kupitia tamasha la leo wamefanyabiashara sana.

“Lakini soko hili la nyama choma litakuwa linaingiza sh.milioni 102 kwa mwaka.Ujenzi wake umegarimu Sh.milioni 729, linauwezo wa kuchukua jumla ya wafanyabiashara 232,”amesema Kumbilamoto alipokuwa akielezea soko hilo ambalo limezinduliwa Mei mwaka huu.

Katika tamasha hilo Benki ya CRDB walikuwa sehemu ya wadau ambao wamedhamini kufanyika tamasha hilo na wametumia nafasi hiyo kutoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo ya kufungulia akaunti wajasiriamali katika soko hilo.

Hata hivyo maofisa wa benki hiyo wameahidi kuendelea kuwa karibu na wajasiriamali katika soko hilo sambamba na kuwapatia mikopo itakayowezesha wajasiriamali hao kuendelea na shughuli zao na kusisitiza kwamba CRDB inasema hivi Ulipo Tupo.

Wakati huo huo wajasiriamali wa soko hilo wametoa ombi tamasha la nyama choma katika soko hilo liwe endelevu kwasababu wamefanyabiashara sana ukilinganisha na siku za kawaida.

“Tumeuza nyama, chakula, vinywaji , matunda na tumeburuduka. Kwakweli tunaomba waandaaji ikiwezekanalifanyike kila mwisho wa wiki,”wamesema.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...