MDAU wa Maendeleo Mkoa wa Iringa, Wakili Sosten Mbendule amempongeza Chifu Adam Sapi Mkwawa II kwa kuwaleta pamoja katika kuadhimisha tamasha la utamaduni la Wahehe.


Wakili Mbedule amesema tamasha hilo la Wahehe lililoanza Juni 16 na kufikia kilele chake leo Juni 19, 2025 katika kijiji cha Kalenga mkoani Iriga linasaidia kudumisha utamaduni wa kabila la Wahehe na kukemea mmomonyoko wa maadili hususani katika suala la mavazi.

Amesema, kuanzishwa kwa tamasha hilo mila, desturi za tamaduni za wahehe zitaimarika kwani zilishaanza kupotea ikiwa ni pamoja na kuhamasisha elimu ya kulinda utu wa mtu.

“Tamasha hili ni lizuri limeleta chachu ya matumizi ya biadhaa za uzalishaji wa kilimo, utalii na huduma mbalimbali za usafirishaji fedha na bima,” amesema.

Pia limesaidia kuwaleta pamoja vijana, wanawake na wazee katika kulinda na kuendeleza urithi wa tamaduni za wahehe nchini.

Katika maadhimisho hayo yamefanyika matambiko ya kimila katika maeneo ya kihistoria ya mto Mkwawa na wahehe kwa ujumla, kutatembelea maeneo ya kihistoria lengo ni kukuza utamaduni wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...