Na Farida Mangube, Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa mauaji ya kikatili yaliyotokea usiku wa kuamkia Juni 21, 2025 katika Kitongoji cha Bombani, kijiji na kata ya Dumila, Wilaya ya Kilosa, ambapo mfanyabiashara wa huduma za kifedha, Mana Selemani Ally (50), aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayedhaniwa kuwa jambazi.

Tukio hilo limetokea wakati marehemu akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kufunga biashara yake ya miamala ya fedha. Inadaiwa kuwa alivamiwa ghafla na mtu huyo ambaye alimpiga risasi na kisha kumpora mkoba mdogo uliodaiwa kuwa na fedha kabla ya kutoweka.

Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi inaesema uchunguzi wa kina unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hilo.

“Tunawaomba wananchi wenye taarifa zozote kuhusu mtu au watu waliohusika na tukio hili watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. Ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kudhibiti matukio ya kihalifu,” imesema

Jeshi la Polisi limeongeza ulinzi na doria katika maeneo ya Dumila na vitongoji jirani, huku likisisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana kwa karibu katika kupambana na uhalifu.

Tukio hili limezua hofu kwa wakazi wa Dumila ambao wameiomba Serikali na vyombo vya dola kuongeza ulinzi hasa nyakati za usiku na kwenye maeneo ya biashara za miamala ya fedha ambazo zimeonekana kuwa shabaha ya wahalifu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...