Na John Mapepele

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa rai kwa walimu nchini kuwa wazalendo na kuzingatia weledi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Mhe. Mchengerwa ametoa rai hiyo kwenye mkutano wa walimu na wadau wa elimu wa Wilaya ya Rufiji uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Bibi Titi Mohamed, ambapo yeye mwenyewe pia alitunukiwa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu wilayani Rufiji.


"Katika hali ya kawaida Serikali imeboresha mazingira na miundombinu ya sekta ya elimu kilichobaki ni kwa sisi walimu kutanguliza uzalendo ili kuinua kiwango cha elimu katika ngazi zote" . Amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Aidha, amesisitiza walimu kutambua wajibu wao na kwamba Serikali haitaweza kusita kuwachukulia hatua za kinidhamu Walimu na Maafisa Elimu ambao watakuwa wazembe katika utekelezaji wa majukumu yao.


Katika taarifa ya Wilaya ya Rufiji kwa Mhe. Waziri, iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Rufiji, bwana Simon Berege, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaohitimu darasa la Saba kutoka 3135 mwaka 2020 hadi wanafunzi 3715 mwaka 2024.

Idadi ya shule za Awali na Msingi zimeongezeka kutoka 48 mwaka 2021 Hadi 63 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la shule 15 sawa na asilimia 31.3. 

Pia vyumba vya madarasa vimeongezeka kutoka vyumba 377 mwaka2921 hadi vyumba566 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la vyumba vya madarasa 189 sawa na asilimia 50. 1

Aidha, katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa, Halmashauri ya Mji wa Rufiji imefanikiwa kushinda kwa nafasi ya kwanza katika michezo ya mpira wa miguu, pete na riadha huku ikishika nafasi ya pili kwenye mpira wa mikono hivyo kushika nafasi ya pili ya ujumla katika mashindano hayo.

Katika mkutano huo Mhe.Waziri Mchengerwa alikabidhi makombe hayo kwa shule na baadaye kupokea msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya CRDB.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...