Na. Peter Haule na Saidina Msangi, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ambaye ni mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma, ameipongeza Wizara ya Fedha na Taasisi zake kwa umahiri katika utoaji huduma alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Pongezi hizo amezitoa baada ya maelezo yaliyotolewa na Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, kuhusu huduma zinazotolewa na Wizara kupitia Idara, Vitengo na Taasisi zake.
Prof. Pallangyo alizitaja huduma zinazotolewa katika Banda hilo kuwa ni pamoja na elimu kuhusu Elimu ya Fedha, Bajeti ya Serikali, Usimamizi wa Mali za Serikali, Pensheni ya Wastaafu inayotolewa na Hazina, Mifumo ya Fedha na Usimamizi wa Deni la Serikali.
Aliongeza kuwa huduma zinazotolewa na Taasisi za Wizara ya Fedha ni pamoja na Program zinazotolewa na Vyuo vilivyo chini ya Wizara lakini pia masuala ya Usimamizi wa Bima, Mifuko ya Uwekezaji na Takwimu rasmi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, aliwataka watumishi wa Wizara ya Fedha, kuendelea kutoa huduma kwa Weledi katika kipindi chote cha maadhimisho hayo ili wananchi wapate uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara zikiwemo Sera na program za Wizara.
Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma imeanza Juni 16 na inatarajiwa kuhitimishwa Juni 23 mwaka huu ikiwa na kauli mbiu ya “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchangia Uwajibikaji”.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiagana na Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, katika Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yenye kauli mbiu ya “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchangia Uwajibikaji”, yanayofanyika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bw. Renatus Msangira, akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Fedha kuhusu huduma wanazozitoa katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama, Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga (wa pili kushoto), akitoa elimu ya Mifumo ya Fedha kwa mkazi wa Dodoma, Bw. Frank Chambua (kulia), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma, yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama, Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga (kulia), akitoa elimu ya Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) kwa wakazi wa Nzuguni jijini Dodoma, Bw. Gideon Katatanama (katikati) na Bruno Sanga, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma, yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (katikati) na Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yenye kauli mbiu ya “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchangia Uwajibikaji”, yanayofanyika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (katikati) na Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Taasisi zake wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yenye kauli mbiu ya “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchangia Uwajibikaji”, yanayofanyika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (katikati) na Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia), akiwataka watumishi wa Wizara ya Fedha, kuendelea kutoa huduma kwa Weledi katika kipindi chote cha maadhimisho Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayofanyika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...