MWENGE wa Uhuru leo umefika katika Wilaya ya Ilala amabpo mwenge huo unataraji kuzindua miradi Saba ya Maendeleo Wilaya ya Ilala, mkoani yenye thamani ya sh bilioni 44 .5 na kukimbia km 82.6. ukiwa pia umebeba ujumbe mzito wa uchaguzi wa Amani.
Akizungumza wakati anakabidhiwa Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alisema miradi hiyo ipo katika mitaa zaidi ya 18, Kata zaidi ya 18 za wilaya hiyo hivyo wananchi watapata fursa ya kuona mwenge na kushuhudia miradi ya maendeleo ikizinduliwa .
mara baada ya kukagua miradi ya Maendeleo Mwenge huo utakwenda kulala katika Viwanja vya Kampala Gongolamboto ambapo msanii maarufu Diamond Platnum atatumbuiza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...