MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Morogoro Mjini, Dkt Ally Simba amekipongeza chama hicho kwa Ilani yake bora ya Uchaguzi inayojali maslahi ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewataka wanachama wote wa CCM kuisoma kwa undani na kuielewa kikamilifu pamoja na kuitangaza hususani wakati huu ambapo Taifa linapokaribia kufanya Uchaguzi wake mkuu wa Oktoba Mwaka huu hatua ambayo itawawezesha wananchi kuielewa na hivyo kukipa ushindi wa kishindo chama hicho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Dkt Simba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano la Afrika Mashariki lenye Makao yake Makuu Kigali, Rwanda alisema ilani hiyo ya uchaguzi Mwaka 2025-2030, imebeba matumaini makubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Alisema ilani hiyo iliyojaa ubunifu mkubwa kwa kuweka vipaumbele vya kila mkoa inatambua kuwa maendeleo lazima yaanzie ngazi ya chini ikionesha kuwa ni kwa namna gani inaheshimu ukweli kwamba "siasa ni ya wananchi wa kawaida", na watu lazima wajione ndani ya ahadi zinazotolewa.

Alisema kimsingi nguzo kuu za Ilani mpya ya Mwaka 2025–2030 inajengwa kwa misingi ya mageuzi ya kisasa ya uchumi jumuishi, shindani na unaotegemea kuongeza thamani ya rasilimali za ndani huku ikiongeza fursa za ajira kwa vijana, kuongeza kipato cha wananchi na kupunguza umaskini.

" Hii ni dira yetu ya kisiasa, tunapaswa kuilinda kwa hoja, shauku, na unyenyekevu wakati wa kampeni.Tuanze Kujipanga kwa Utekelezaji wake, wana CCM tuna kila sababu ya kuamini kuwa kwa Ilani hii, Mgombea wetu wa nafasi ya Urais, Dkt Samia Suluhu Hassan na Mgombea mwenza wake, Dkt Emmanuel John Nchimbi wataibuka na ushindi wa kishindo"

"Aidha, tuna kila sababu ya kuamini kuwa CCM itakuwa chama chenye wabunge wengi bungeni na kuunda serikali, hivyo basi, sasa ni wakati sahihi wa kuanza kufikiria utekelezaji wake, shangwe nilizoshuhudia ndani na nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete ni lazima zilingane na nidhamu, mipango madhubuti na azma ya pamoja ya kutekeleza Ilani hii kwa manufaa ya Watanzania wote" alisema Dkt Simba

Pamoja na hiyo ilani hiyo pia imezingatia kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii kwa kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji sambamba na kukuza matumizi ya sayansi na teknolojia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi huku ikidumisha demokrasia na utawala bora.

"Tuna kila sababu ya kuamini kuwa CCM itakuwa chama chenye wabunge wengi bungeni na kuunda serikali, hivyo ni wakati sahihi wa kuanza kufikiria utekelezaji wake. Shangwe nilizozishuhudia ndani na nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete ni lazima zilingane na nidhamu, mipango madhubuti na azma ya pamoja ya kutekeleza Ilani hii kwa manufaa ya watanzania wote" alisema Dkt. Simba

Alisema kimsingi Ilani hiyo inazungumza lugha ya kawaida, inagusa mahitaji ya kila mwananchi na kuakisi falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya “Kazi na Utu” ikimuasa kila mtu kufanya kazi kwa kuheshimu na kuthamini utu wa kila mmoja. "Iwapo awali alikuwa mlezi wa Ilani iliyopita, basi hii ni uhalisia wake, ndoto yake, na urithi anaotamani kuuacha kwa vizazi vijavyo" aliongeza

Alisisitiza kuwa kwa kiasi kikubwa, tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameanza kujenga urithi huo kwa vizazi vijavyo akiwepo binti yangu Rafat mwenye umri wa miaka 11 ambaye kwa kutambua mchango wa Rais huyo ameandika kitabu chake kinachoitwa “The First Female President”, akihamasishwa na Utendaji na uongozi wa Rais Samia.

"Nilijiuliza nini kilimvutia sana binti yangu na kwamba aliona nini ambacho mimi sikukiona..?, ila baada ya kuhudhuria kwa siku mbili Mkutano Mkuu Maalum wa CCM jijini Dodoma, na kushuhudia uzinduzi wa Ilani, nilielewa vyema nini tafsiri ya kilichokuwa katika akili na fikra za Binti yangu" alisema Dkt.Simba

Alisema ujasiri, uwazi na hekima ya kitaifa ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inamfanya kuwa zaidi ya muhamasishaji na mbadilishaji wa mustakabali wa taifa hivyo kitendo cha binti yangu kulitambua hilo kabla yangu, kunazidisha heshima yangu kwa Rias Samia.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwahamasisha mamilioni ya watanzania kutokana na uongozi wake imara huku akiahidi kuandamana naye kwenye safari ya kuwapatia watanzania heshima, fursa, na mshikamano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...